JESHI la  polisi  mkoa  wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama    vya siasa  kwa vyama  vyote na sio kwa chama  cha Demokrasia na   maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote  kutii sheria bila    shuruti.
Hata  hivyo jeshi  hilo la Polisi  limesema  kuwa   halifanyi kazi kwa  matakwa ya chama  chochote cha  siasa na kuwa si   kweli kama wanavyodai  viongozi  wa Chadema  kuwa  jeshi la polisi   linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano  hiyo.
Kamanda     wa  polisi  wa  mkoa  wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli  hiyo   leo ofisini  kwake  alipozungumza na  waandisha  wa habari  kuhusu    zuio la mkutano  wa Chadema   uliopangwa  kuanza leo  katika  wilaya ya  Mufindi.
"  Nawatangazia  wanasiasa na vyama  vyote  vya siasa  pamoja na  wananchi  wa mkoa  wa Iringa  kuwa  hakutakuwa na mikutano   ya kisiasa kutokana na  shughuli za sensa  zinazoendelea ....hivyo basi  nawaomba  wananchi wote  kutoshiriki mikutano yoyote ya  kisiasa  itakayoitishwa na wanasiasa  "alisisitiza
Kuwa  mikutano  hiyo   imezuiliwa  kwa  kipindi   hiki cha  sensa  kilichoongezwa hadi hapo  tamko litakapotolewa tena  na  msajili wa vyama  vya siasa John Tendwa  kama  alivyokwisha  kutoa tamko  la kuzuia  shughuli  hizo  za vyama   vya siasa kwa  kipindi  hiki cha   sensa.
"Wananchi wote wa  mkoa   wa Iringa mnaombwa  kutii sheria  bila  shuruti  hii ni amri  ....nawaombeni sana  wananchi   kutodanganywa na  wanasiasa  kwa   kuvunja sheria "aliongeza kamanda  huyo  wa  polisi.
Hata   hivyo   alisema  kuwa  kimsingi  zoezi la  sensa  lilipaswa   kuhitimishwa  Septemba mosi mwaka  huu ila kutokana na  serikali  kuongeza  muda wa   zoezi hilo bado jeshi  hilo la polisi  linazingatia  maagizo ya Msajili  wa vyama  vya siasa kama alivyoyatoa kwa  jeshi hilo.
Kamanda   Kamuanda  alisema  kuwa jeshi  hilo la polisi wala msajili wa vyama    vya  siasa hajazuia  vyama  vya  siasa  kuendelea  na vikao vyao  vya   ndani kwa  kipindi  hiki na kuwa hata  Chadema wakiwa mkoani Iringa    wameendelea  kufanya vikao  vyao  vya ndani katika kata mbali mbali za   mkoa  wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia  kuendelea  kufanya   hivyo.
                      -