Mmarekani Chris Wilde akiwa amesimama mahala alipomalizia mbio za  kilometa 50 kama zawadi kwa uhuru wa Tanganyika. Kulia kwake ni  mkimbiaji wa kimataifa wa Tanzania Nelson Brighton.
  -- 
  Chris  Wilde raia wa Marekani aliyekimbia kilometa 50 kuipa Tanzania zawadi ya  miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika ameahidi kurejea tena mwakani kukimbia  kilometa 51 katika mbio za kutimiaza miaka 23 tangu kuanzishwa kwa mbio  za Mt. Kilimanjaro Marathon 1991.
  Wilde  ambaye ni mganga msaidizi kutoka jimbo la Minnesota amekuwa mtu wa  kwanza kukimbia kilometa 50 kusheherekea uhuru wa Tanganyika alipokimbia  katika mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon jumapili tarehe 24 mjini Moshi.
  Mbio  hizo zilifanyika kuanzia Moshi Club hadi Rau madukani na kurudi. Chris  Wilde alirudi mara 9 na nusu ili kutimiza kilometa 50 kama zawadi kwa  nchi ya Tanzania.
  “Naipenda  sana Tanzania na ili kuidhihirishia dunia kuwa mlima Kilimanjaro uko  Tanzania, nakimbia mbio hizi kama zawadi kwa Tanzania” alisema mzungu  huyo mwenye umbo la mwariadha wakati anajiandaa kukimbia mbio hizo  jumapili tarehe juni 24.
  Wilde  aliongozana na mwanariadha wa kimataifa mtanzania Nelson Brighton na  ambaye anakwenda nchini Marekani mwezi ujao kushiriki katika mbio  mbalimbali zilizoandaliwa kwa ufadhili wa Mt. Kilimanjaro Marathon 1991.
  Kumiminika  kwa wakimbiaji wa Kimarekani, Ulaya, Australia, Canada na Scandinavia  katika mbio za Mt. Kilimanjaro marathon ni neema kubwa kwa taifa hili  ambalo lina hazina kubwa sana ya wanamichezo wanaotakiwa kuendelezwa.Chris  Wilde aliungana na mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz  kushiriki katika mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon na kuzifanya kuwa mbio  zinazovutia washiriki wa Kimataifa. Mt. Kilimanjaro Marathon  zilianzishwa mwaka 1991 na Marie Frances kutoka Bethesda nchini  Marekani.
  Ni  mbio zilizokwisha kupewa tuzo na majarida mbalimbali yanayoheshimika  duniani kama vile Wonders of World ambalo lina wasomaji zaidi ya milioni  5 ambalo lilizipa nafasi ya pili wakati ambapo jarida linaloheshimika  la Forbes lilizipa nafasi ya kwanza kama mbio zinazovutia.
  Imetumwa na;
  Grace Soka
  Afisa Uhusiano
  Mt. Kilimanjaro Marathon 1991