Pages

Tuesday, July 3, 2012

Vodacom Tanzania Katika Maonesho ya Sabasaba 2012

Wakala wa Vodacom M PESA akitoa huduma ya M- PESA kwa mteja alietembelea maonesho ya sabasaba jijini Dar es salaam Kampuni ya Vodacom Inashiriki katika maonesho hayo kama mdhamini rasmi wa mawasiliano.
Wateja waliojitokeza katika maonesho ya biashara ya Kimaifa Dar Es salaam (sabasaba) wakipewa maelekezo na wafanyakazi wa kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania,namna ya kutumia simu ya ZTE 502 inayouzwa kwa shilingi elfu 13 katika maonyesho hayo.
Mteja aliejitokeza katika maonesho ya sabasaba akipata maelezo ya namna ya kutumia simu ya ZTE 502 pia iliyokuwa na muda wa maongezi wa shilingi elf 6000 na kuuzwa kwa shilingi elfu 13 ikiwa ni ofa maalum katika maonesho hayo ya sabasaba.
Wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania wakimpa maelekezo mteja alienunua simu aina ya ZTE 502 inayouzwa kwa shilingi elfu 13 katika maonesho ya Biashara ya kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam

Popular Posts