Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la  Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot  akimkabidhi barua  Mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari  Azania  Rahim Rajab ambaye ni mmoja wa kati ya wanafunzi wawili wajumbe  wa UN Clubs waliochaguliwa kuhudhuria Kongamano la maadhimisho ya siku  ya kuzaliwa Rais wa Zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela  litakalofanyika Johannesburg Afrika Kusini ambayo huadhimishwa kila  mwaka Julai 18.
  Wanafunzi hao wamepewa duhamini wa Tiketi za kwenda na kurudi na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (South African Airways-SAA).
 
 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo  la Umoja wa Mataifa nchini  (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akimkabidhi  barua  ya kuchaguliwa kushiriki Kongamano hilo Afrika  Kusini Mwanafunzi  wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa  Nuru Kessy  ambaye ni Mwanachama wa Un Clubs.
 
  Bw. Phillippe Poinsot (kulia)  akimfafanulia Mwanafunzi Nuru Kessy kuwa katika Kongamano hilo  watakutana na wanafunzi wenzao kutoka mataifa mbalimbali duniani wenye  umri kati ya miaka 13-18 na kuwa wanahitaji kufanya utafiti kuhusiana na  maisha ya Mandela ikiwemo miaka ya mwanzo, maisha yake ya jela, maisha  ya uraisi kama mtu aliyepokea tuzo ya Amani ya Nobel, kustaafu kwake na  mchango wake kama kiongozi maarufu duniani.
 
   Wanafunzi hao wakitoa shukrani kwa  Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw.  Phillippe Poinsot (kulia) na Head, Management Support Strategy and  Partnership wa UNDP Ishmael Dodoo (kushoto).
 
  Wanafunzi ambao ni wananchama wa UN  Clubs wanaoelekea Afrika Kusini katika Kongamano la maadhimisho ya siku  ya kuzaliwa ya Nelson Mandela kwa udhamini wa shirika la Ndege la Afrika  Kusini (SAA)  katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa UNDP. Kushoto ni  Reference Assistant kutoka kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC)  Harriet Macha, IT Associate Alice Chopeta, Head, Management Support  Strategy and Partnership wa UNDP Ishmael Dodoo, Wanafunzi Rahim Rajab na  Nuru Kessy, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa  nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot na Information Officer UNIC Stella  Vuzo.