Mkurugenzi   Mtendaji wa MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS Bw. Walter Bugoya akitoa neno   wakati wa uzinduzi wa kitabu cha 'FURAHA HUJA ASUBUHI' (JOY COMES IN THE   MORNING) kilichoandikwa na Hopolang Phororo kinachozungumzia Mateso na   manyanyaso ya wasichana wadogo wakati wa malezi yao na haki ya msingi  ya  jinsia ya kike katika jamii.
 Mmoja   wa washiriki wa uzinduzi huo Bi. Chansa Kapaya akitoa neno la shukrani   wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Hopolang Phororo na haki za msingi za   wanawake wanaokutwa na matatizo ya unyanyasaji wa Kijinsia Tanzania.
 Mtunzi   wa Kitabu cha 'JOY COMES IN THE MORNING' Bi. Hopolang Phororo  akielezea  simulizi ya kweli iliyomkuta kama mwathirika wa unyanyasaji  wa Kijinsia  wakati wa usichana wake na moyo, uvumilivu aliokuwa nao wa  kuweka  uzoefu huo katika maadishi ili jamii ijifunze na madhara ya  unyanyasaji  wa Kijinsia unaokua kwa kasi nchini Tanzania.
Mgeni   rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Fatma Mrisho akitoa nasaha   zake wakati uzinduzi rasmi wa kitabu hicho jijini Dar es Salaam. Alisema   66% ya wanawake na 20% ya wanaume nchini wameshawahi kukutwa na  majanga  ya unyanyasaji wa Kijinsia  katika maelzi yao ambapo kwa sasa  Dar es  Salaam na Mbeya zinaongoza.
 Mgeni   rasmi Dkt. Mrisho na Mtunzi wakionyesha Kitabu kwa wageni waalikwa na   waandishi wa habari. Kitabu hiki kinapatikana katika Maduka ya MKUKI NA   NYOTA PUBLISHERS  yaliyopo jijini Dar es Salaam kwa gharama ya  shilingi  10,000/=.
 Jopo la Wataalam wa Mambo ya Jinsia Tiba na Vitabu wakiwa kwenye picha pamoja.
 Mkurugenzi wa MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS Mzee Bugoya akibadilishana mawazo na Dkt. Mrisho pamoja na Bi. Kapaya wakati wa uzinduzi
 Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa kitabu cha 'JOY COMES IN THE MORNING' uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo baada ya uzinduzi.