
Marehemu Kardinal Laurean Rugambwa enzi ya uhai wake.
Kanisa kuu katoliki jimbo la Bukoba ambalo masalia ya marehemu kardinali Rugambwa yatazikwa ndani yake.
*************
MWILI WA KARDINALI LAUREAN RUGAMBWA  KUZIKWA UPYA OKTOBA 6, BUKOBA 
Kanisa   katoliki nchini dayosisi ya Bukoba mkoani Kagera, wanajiandaa kuzika   upya masalia ya mwili wa aliyekuwa askofu wa dayosisi hiyo Kardinali   Laurean Rugambwa, aliyefariki mnamo mwaka 1997 katika kanisa kuu la   Bukoba. Maziko ya Kadinali Rugambwa yamepangwa kufanyika siku ya oktoba 6   mwaka huu.
Mwili   wa askofu huyo wa kwanza nchini na Kardinali wa kwanza mweusi barani   Afrika umezikwa katika kanisa la kwanza mkoani Kagera lililopo Kashozi   kutokana na kwamba kanisa kuu la Bukoba ambalo marehemu aliagiza   kuzikiwa ndani yake lilikuwa katika matengenezo makubwa.
Akizungumza   katika kipindi cha Baragumu Channel ten na baadaye kwenye mkutano na   waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Askofu msaidizi wa Jimbo la   Bukoba Askofu  Methodius Kilaini , amesema wanataka kumzika kardinali   Rugambwa kwa heshima tena katika kanisa alilopenda kuzikiwa kutokana na   kukamilika kwake, lakini kabla ya kuzikwa humo kutatanguliwa na ibada   mbalimbali ikiwa sehemu alikozaliwa, alikobatizwa, sherehe   zitakazoambatana na kusherehekea miaka 100 ya kuzaliwa kwa kardinali   Rugambwa tarehe 7 mwezi Octoba.
"tuna   alika watu wengi kuhudhuria kwenye tukio hili..., na pia tunakaribisha   michango itakayowezesha kuwa na kitu cha kumkumbuka marehemu kwa  mchango  wake,alisema askofu Kilaini.
Naye   mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya kufanikisha tukio hilo ,   James Rugemalira, alimwelezea Kardinali Rugambwa kama mtu aliyetoa   mchango mkubwa kwenye jamii ya watanzania, kuanzia kwenye nyanja za   elimu, afya na kiroho.
Marehemu   Kardinali Rugambwa ana mambo mengi ya kukumbukwa na jamii ya  watanzania  hususani watu wa mkoa wa Kagera hasa kwa juhudi zake za  kupeleka elimu  mkoani humo kwa kuagiza ujengwaji wa shule za msingi na  sekondari  ikiwemo shule ya kwanza ya wasichana ya Rugambwa ambayo  ujenzi wake  ulikuwa ni mafanikio ya marehemu huyo kuomba msaada wa  ujenzi wa shule  hiyo alipohutubia bunge la Ujerumani akiwa mwafrika wa  kwanza.
Licha   ya mambo hayo yote kanisa hilo pia liko mbioni kuanzisha mfuko rasmi  wa  kumuenzi kardinali huyo mfuko utakaojulikana kwa jina la Kardinali   Rugambwa ambao utakuwa maalumu kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali   za kijamii.
Padre   Laurean Rugambwa aliwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 10   Februari,1952. Alizaliwa julai 22 1912 na kufariki miaka 15 iliyopita.