Pages

Tuesday, September 11, 2012

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa Akabidhi madawati 500 kwa shule ya msingi minazi mirefu iliyopo Ukonga jijini Dar es Salaam

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akikata utepe wakati wa makabidhiano ya madawati 500 kwa shule ya msingi minazi mirefu iliyopo Ukonga jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mahusiano ya Serikari wa Kampuni ya African Barrick Gold, Emmanuel Ole-Naiko
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akizungumza katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Mahusiano ya Serikari wa Kampuni ya African Barrick Gold, Emmanuel Ole-Naiko wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 500 katika Shule yua Msingi Minazi Mirefu iliyopo Ukonga jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akitizama wanafunzi wakiwa wamekalia madawatimuda mfupi baada ya kukabidhi 500 kwa shule ya msingi minazi mirefu iliyopo Ukonga jijini Dar es Salaam jana.

Uzinduzi wa Bodi Mpya Ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi (GEPF)

Katibu Mkuu Wizara ya fedha, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhan Khijah akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi mpya wa wakurugenzi ya Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi (GEPF) uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Akiba ya wafanyakazi GEP, Daud Msangi na Mwenyekiti mpya wa bodi ya GEPF, Joyce Shahidi.
Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Daud Msangi akizungumza
Meneja Masoko wa GEPF, Aloyce Ntukamazina akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo
Mwenyekiti wa bodi iliyomaliza muda wake ya Mfuko wa wa Akiba ya Wafanyakazi (GEPF), iliyomaliza muda wake, Monica Mwamunyange akizungumza katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha,Ramadhan Khijah akimkabidhi zawadi,Mwenyekiti wa bodi iliyomaliza muda wake ya Mfuko wa wa Akiba ya Wafanyakazi (GEPF), Monica Mwamunyange kutokana na mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha uongozi wake.Picha Zote na Dande JR

MAKAMU WA RAIS DKT.GHARIB BILAL AKUTANA NA UJUMBE WA KAMATI YA PARLIAMENTARY UNITY (IPU)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Akiagana na Mbunge wa Bunge la Zimbabwe na Mjumbe wa Kamati ya Interparliamentary unity (IPU), Thabitha Khumalo, wakati akiagana na ujumbe wa IPU baada ya mzungumzo na ujumbe huo, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Sept 11, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na ujumbe wa Kamati ya ‘Interparliamentary Unity’ (IPU), wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Sept 11, 2012 kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Kamati ya Interparliamentary unity (IPU) baada ya mazungumzo wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Sept 11, 2012. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Maandamano ya Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Leo Kupinga mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi

Waandamanaji wakielekea Jangwani.
Waandishi wa habari wakiandamana kuelekea kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo.
Jane Mihanji kutoka gazeti la Uhuru akitoa salam zake leo wakati wa kuhitimisha maandamano ya waandishi wa habari kupinga kuuawa kwa mwandishi mwenzio Daudi Mwangosi.
Mhariri Mkuu wa NIPASHE, Jesse Kwayu akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari kufuatia maandamano ya kupinga mauaji ya David Mwangosi (katika picha kulia) kwenye viwanja vya Jangawani, jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo.
Waziri wa mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi akiondoka viwanja vya Jangwani baada ya kutakiwa kuondoka na waandishi wa habari.
Waandishi wakiigiza kile kilichomkuta mwenzao mbele ya polisi
Waandishi wakisapoti jambo wakati wa mkutano wao baada ya maandamano ya kupinga mauaji ya David Mwangosi asubuhi ya leo
Mwandishi mkongwe Hamis Mzee akichukua matukio muhimu wakati wa maandamano hayo.
Mwanzo Milinga akichukua baadhi ya matukio muhimu.Picha na Straika na Mdau Adam Mzee
---
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, amekumbana na fadhaa ambayo haikutarajia wakati alipotimuliwa katika maandamano ya waandishi wa habari ya kupinga mauaji ya mwandishi mwenzao wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, David Mwangosi, wakati alipozuka bila mwaliko.

Huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofauti, waandishi waliandamana kuanzia kwenye ofisi za Channel Ten katikati ya jiji la Dar es Salaam na kutembea hadi katika viwanja vya Jangawani lakini walipofika mwisho wa maandamano yao walipigwa na butwaa baada ya kumkuta Waziri Nchimbi akiwa wa kwanza kufika katika eneo hilo tayari kupokea maandamano.

Wakati Nchimbi akijiandaa kuanza kuzungumza mbele ya wanahabari, upinzani mkali ukazuka kwa waandishi dhidi ya kiongozi huyo wa serikali wakitaka aondoke mahala hapo kwani maandamano hayo yalikuwa hayamuhusu.

"Atokee.... aondokee.... hatumtakiiii.... nani kamleta hapa?" yalikuwa ni baadhi ya maneo yaliyokuwa wakitolewa kwa sauti kubwa kupinga uwapo wa waziri Nchimbi mahala hapo.

Huku akizomewa, Waziri Nchimbi alijaribu kuvumilia aibu hiyo kwa takriban dakika tano huku pengine akitumai kwamba watamruhusu kuzungumza kilichompeleka mahala hapo.

Mwandishi wa habari mkongwe, ambaye pia ni mwanasheria, Nyaronyo Kicheere, alisogea mbele ya umati wa waandishi na kusimama jirani na alipokuwapo waziri Nchimbi na kusema: "Tumeambiwa tunakuja hapa kwa ajili ya mkutano wa waandishi wa habari na utapokewa na jukwaa la wahariri, inakuwaje tupokewe na mtu mwingine. Hatumhitaji mtu mwingine hapa, aondoke."

Baada ya kauli hiyo, waziri Nchimbi aliondoka mahala hapo na kuzua shangwe kubwa kwa waandishi ambao pia walimsindikiza kwa kumzomea mpaka alipoingia katika gari lake la wizara. Hakuja na gari lake la waziri.

Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari walizungumza na kukemea mauaji hayo na bila ya kuuma-uma maneno walisema kwamba Mwangosi aliuawa kwa kulipuliwa na polisi na kwamba waliohusika wote wachukuliwe hatua za kisheria.

"Waandishi na wafanyakazi wengine wanalipa kodi ilipolisi wapate magwanda, wapate bunduki, wapate mabuti na wanalipwa ili walinde raia na sio kuua raia, vitendo kama hivi havikubaliki," alisema Jesse Kwayu, mhariri mkuu wa gazeti la NIPASHE.

Mwandishi mkongwe, Masoud Sanani, aliongeza: "Waarabu wanasema 'wal kiswaswa haq' yaani 'kisasi ni haki', lakini sisi kwa busara tunasema kwamba hatuna kisasi ila tunataka mambo haya yawe mwisho, waandishi waachwe wafanye kazi zao kama askari wanavyoachwa wafanye kazi zao."

"Tumeshasikia askari akitingishwa kidogo, mtu anashitakiwa kwa kumzuia askari kufanya kazi yake, tunataka waandishi nao waachwe wafanye kazi yao," alisema.

Waandishi walitaka familia ya marehemu Mwangosi ilelewe na watoto wasomeshwe mpaka watakapofikia.

Miongoni mwa mabango yaliyokuwapo katika maandamano hayo yalisomeka: "Bunduki na mabomu hayatazuia kalamu zetu kuandika ukweli," "Hatuogopi vitu vizito wala vitu vya ncha kali"....


Yalikuwa ni maandamano ya amani. Hapakuwa na vurugu zozote na askari waliokuwapo wengi walikuwa mikono mitupu bila ya silaha yoyote hata virungu ukiacha wachache waliobeba silaha na askari wa usalama barabarani waliongoza maandamano wakizuia magari wakati waandishi wakipita katika njia zote kuelekea kwenye viwanja vya Jangawani.

Monday, September 10, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT GHARIB BILAL AFUNGUA MKUTANO WA WA SABA WA WALIMU WA AFRIKA (African Confederation for Principles (ACP).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa siku 3 kwa walimu wa nchi za Afrika unaojadili kuboresha Elimu kwa nchi za Afrika. Mkutano huo unahudhuriwa na wawakilishi wa walimu kutoka nchi saba za Afrika zinazotumia lugha ya Kiingereza katika ufundishaji. (Tarehe 10,Septemba 2012)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa siku 3 kwa walimu wa nchi za Afrika unaojadili kuboresha Elimu kwa nchi za Afrika. Mkutano huo unahudhuriwa na wawakilishi wa walimu kutoka nchi saba za Afrika zinazotumia lugha ya Kiingereza katika ufundishaji. (Tarehe 10,Septemba 2012)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaaga walimu kutoka nchi za Afrika wanaohudhuria mkutano wa 7 wa ACP, unaojadili kuhusu maboresho ya Elimu kwa nchi za Afrika. Mkutano huo umefunguliwa leo na Mheshimiwa Makamu wa Rais na unahudhuriwa na wawakilishi wa walimu kutoka nchi saba za Afrika hususani zile zinazotumia lugha ya Kiingereza katika ufundishaji.(Tarehe 10, Septemba 2012).Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Popular Posts