
 Waziri  wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Theresia Huvisa  akizungumza na wandishi wa habari jijini Arusha leo kuhusiana na  maandalizi ya mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Mazingira kutoka barani  Afrika Tanzania ikiwa mwenyeji wa mkutano huo.
--- 
Na.MO  BLOG -Arusha
Waziri  wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  (Mazingira) nchini Tanzania Mh.  Theresia Huviza anatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa Rais wa Mazingira kwa  Afrika katika Mkutano wa 14 wa Mawaziri wa mazingira unaofanyika Arusha  nchini Tanzania kuanzia kesho hadi tarehe 14 mwezi huu. 
Waziri Huviza ataongoza kwa kipindi cha muda wa miaka miwili ambapo baada ya hapo nafasi hiyo itachukuliwa na nchini nyingine. 
Mkutano  huo umefanikishwa na European Union, Ubalozi wa Norway, Global  Environmental Facility, UNEP na UNDP na wajibu mwingine ukifadhiliwa na  serikali yenyewe.Bajeti ya maandilizi ya mkutano huo imegharimu takriban   dola za kimarekani 350,000 sawa na shilingi za Tanzania zaidi ya  milioni mia 6.

Pichani  juu na chini ni Watoto wakifanya mazoezi ya wimbo maalum watakaoimba  kesho kwenye mkutano wa 14 wa mawaziri wa mazingira barani Afrika mbele  ya Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  (Mazingira) nchini Tanzania  Mh. Theresia Huviza.


Harriet  Macha kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(kushoto) akitoa  maelezo mmoja wa wadau wa mazingira aliyefika katika banda la Umoja wa  Mataifa lililopo katika jengo la AICC utakapofanyika mkutano wa 14 wa  mawaziri wa Mazingira.

Afisa  Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu aktioa maelezo kwa  mmoja wa wadau ya namna Umoja wa Mataifa inavyoshirikiana na Serikali ya  Tanzania katika utunzaji wa Mazingira kupitia mpango wa mazingira  (UNEP) uliopo chini ya Umoja wa Mataifa.

Banda  la ROA OZONE ACTION PROGRAMME chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais na UNEP  wakitoa maelezo katika kutunzaji wa mazingira kwa wananchi.