Pages

Friday, August 3, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AGAWA NGOMBE 500




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha (Longido,Monduli na Ngorongoro) kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.Kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo hilo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Kushoto kwake ni WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.

Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli mchana wa leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa shukrani kwa Mh. Rais Jakaya Kikwete kwa kuweza kuwakumbuka wananchi wa Wilaya ya Mbonduli.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigawa Ng'ombe kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.



Wananchi wa Kijiji cha Makuyuni wakifatilia zoezi la ugawaji wa Ng'ombe.


Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa alipowasili katika kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli kwa ajili ya kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.


Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Arusha waliofika katika kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli kumlaki.Rais Kikwete leo amefika katika kijiji hicho cha Makuyuni na kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha (Longido,Monduli na Ngorongoro) kama kifuta jasho cha kupoteza mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake zilizotokea mwaka 2008/2009.





Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.



Rais Kikwete akielekea kwenye Jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya kuwahutubia wananchi wa Monduli

Wananchi wa Kijiji cha Makuyuni Wakizungumza
Wananchi wa Kijiji cha Makuyuni wakifatilia zoezi la ugawaji wa Ng'ombe.


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipatiwa maelezo ya Mifugo hiyo kabla Rais Kikwete hafafika na kuigawa kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake uliozikumba wilaya hizo mwaka 2008/2009.



Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika Mazungumzo na Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh. Christopher Ole Sendeka.Picha na IKULU
---
SERIKALI itakuwa inagawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha karibu mifugo 800,000 iliyopotea kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
Ahadi hiyo imetolewa jana, Alhamisi, Agosti 2, 2012 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipozindua Mradi wa Serikali wa Uwezeshaji Mifugo kwa waliopotelewa mifugo yote katika Wilaya ya Monduli kwenye sherehe iliyofanyika Makuyuni wilayani humo.
Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi wa Mkoa wa Arusha wakiwemo wakuu wa wilaya na wabunge wa mkoa huo, Rais Kikwete amegawa ng’ombe 500 kwa kundi la kwanza la wananchi ikiwa ni mitamba minne na dume moja la kisasa kwa kaya 16 za mwanzo.
Uzinduzi huo ni wa pili kufanywa na Rais Kikwete chini ya Mradi huo wa kwanza wa aina yake kubuniwa na Serikali katika historia na wenye thamani ya sh. Bilioni 12.9.
Februari 19, mwaka huu, Rais Kikwete alizindua Mradi kama huo katika Wilaya ya Loliondo kwenye sherehe zilizofanyika mjini Loliondo. Kesho Agosti 3, 2012 Rais Kikwete anatarajiwa kuendelea na zoezi hilo katika mji wa Loliondo

Popular Posts