Pages

Sunday, August 26, 2012

KIKUNDI CHA SERENGETI CHAJIUNGA NA CHADEMA


Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Arusha Mh Samson Mwigamba.
Katibu wa Chadema wa mkoa wa Arusha Mh Amani Golugwa.
Mmoja wa Viongozi wa Kikundicha Serengeti akikabidhiwa katiba ya Chadema.
Wasanii wa kikundi cha Serengeti walioamua kujivua gamba na kujiunga na Chadema.Picha na Habari na CHADEMA
---
Sanaa kama moja wapo ya vyanzo vya ajira nchini haina budi kusimamiwa kikamilifu na serikali ili kuwezesha taifa kupunguza tatizo la ajira. Ni wakati muafaka hivi sasa kwa serikali kuhakikisha inaandaa utaratibu mzuri wa kukulinda maslahi ya wasanii kwa kusimamia uendeshwaji mzima wa biashara ya kazi hizo.Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa wa Arusha, Mwigamba Samson wakati akiwapokea wanachama zaidi ya 40 ambao ni wasanii wa kikundi cha Serengeti Art Group kama wanachama wapya wa chama hicho.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa inashangaza kuona wasanii wengi wa Tanzania wana hali mbaya kiuchumi licha ya kazi kubwa na nzuri wanazozifanya na kuongeza kuwa hali hiyo inasababibshwa na serikali iliyopo madarakani kutojali kazi hizo. Amesema kama chama na kupitia wabunge wa chadema wamefanya kazi kubwa ya kuishinikiza serikali kuliona hilo na kulifanyia kazi.

Kwa upande wake Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha Amani Golugwa, amesema sera ya chama chake kuhusu sanaa ni kuona kuwa sanaa haibakii kutumbuiza peke yake bali ni kuhakikisha kuwa inakua ajira rasmi kwa wasanii na wadau wanaojihusisha nayo kwa namna moja ama nyingine.

Katibu huyo ameongeza kuwa vuguvugu la mabadiliko linaloendelea hivi sasa lina lengo la kuzidi kukiimarisha chama na kwamba mkoani Arusha vuguvugu hilo litafanyika mnamo mwezi wa kumi na moja hivyo amewataka wanacham hao wapya kuanza kazi ya kuleta mabadiliko kama lengo la vuguvugu hilo linavyosema.

Popular Posts