Waandishi  wa mitandao ya kijamii na tovuti kupewa tuzo kutokana na jitihada na  mafanikio yao. Tuzo hizo kuitwa “ Tuzo za umahiri wa digitali za  Vodacom”Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, itatoa tuzo kwa  waandishi bora kumi mahiri katika mitandao ya kijamii kutokana na  umahiri wao.
  Tuzo  hizo ambazo zimepewa jina la “Tuzo za Umahiri wa Digitali za Vodacom”,  zitatolewa kwa washindi kumi kutokana na jitihada zao na mafanikio yao  ikiwa ni kwa mala ya Kwanza kufanywa na kampuni ya simu za Mkononi ya  Vodacom.
  Mkurugenzi  mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema kuwa  Waandishi wa mitandao ya kijamii wanao mchango mkubwa katika kutoa  taarifa mbalimbali ndani ya jamii, na mchango huu unatakiwa kuthaminiwa.
  Wapo  waandishi wengi katika mitandao ya kijamii na wanaandika masuala  mbalimbali kuhusu biashara au hata yale yanayogusa jamii moja kwa moja,  Ni kwa sababu hii ndio maana tunatambua na kuwapatia tuzo hizi kutokana  na mabadiliko waliochangia katika utoaji wa taarifa” Alisema Meza.
  Baadhi  ya sifa ambazo zitapewa kipaumbele katika tuzo hizi, pamoja na mambo  mengine, ni ubunifu na utoaji wa taarifa za kijamii, Kuzingatia ueledi  wa uandishi na uhuru wa vyombo vya habari, mahusiano na wasomaji katika  utoaji wa taarifa, umahiri wa picha na ushirikishwaji wa vyombo  vingingine.
  Waandishi  wa mitandao ya kijamii wata shindanishwa kadri inavyowezekana ili  kuwawezesha kuongeza ueledi na umahiri katika kazi zao.
  Kampuni  ya Vodacom Tanzania pia itaanzisha mfuko wa fedha wa maendeleo ya  digitali, Kwa mujibu wa Meza fedha hizi zitatumika katika kuendeleza  umahiri na kuboresha kazi katika mitandao ya kijamii na tovuti.
  “Huu  ni mchango kutoka Mfuko wa M-pesa ambapo waombaji wataweza kuzitumia  katika udhamini na kuendeleza shughuli zao”, Alisema Meza na kuongeza  kuwa, “ Tunathamini mchango wa kila mtu, na tunahitaji waandishi wa  mitandao ya kijamii wote waendelee kufanya kazi zao nasi tutaendelea  kuthamini na kutambua mchango wao na kuwapa tuzo.”
