

  Pichani juu na chini ni  Balozi wa  Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo akiongea machache kwenye  hafla fupi ya kutimiza miaka 35,mbele ya wageni waalikwa mbalimbali  wakiwemo mabalozi kutoka sehemu mbalimbali,hafla hiyo imefanyika jioni  ya jana nyumbani kwa balozi huyo,jijini Dar.
 
 Sehemu ya baadhi ya wageni waalikwa  wakisikiliza hotuba fupi iliyokuwa ikitolewa na Balozi wa Jamhuri ya  Djibouti, Saidi Amin Shamo,kwenye hafla fupi ya kutimiza miaka 35 ya  jamhuri ya Djibout iliyofanyika jioni ya jana jijini Dar.
 
 Wageni waalikwa wakijadiliana jambo,Pichani kati ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Bw.Joseph Kusaga.
 
 Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa  wamekusanyika nyumbani kwa Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi  Amin Shamo,wakisherehekea hafla fupi ya  kutimiza miaka 35 ya jamhuri  ya Djibout iliyofanyika jioni ya jana jijini Dar.
 
 Burudani kama hivi ilikuwepo kwa wageni waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo.
 
  Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania,  Saidi Amin Shamo akimpokea mgeni rasmi wa hafla hiyo,Rais mstaafu wa  awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi alipokuwa akiwasili nyumbani kwa  balozi huyo.
 
  Balozi wa Jamhuri ya Djibouti, Saidi  Amin Shamo  akimkaribisha Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri  kuwa Mwanachama wa Freemasons) mara alipokuwa akiwasili kwenye hafla  hiyo.
 
 Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons)  akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi  jioni ya jana kwenye viunga vya balozi wa Jamhuri ya Djibouti, Saidi  Amin Shamo
 
 Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania,  Saidi Amin Shamo akizungumza machache na machache na Rais mstaafu wa  awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi ,shoto ni Sir Andy Chande (Mtanzania  wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons)
 
 Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania,  Saidi Amin Shamo sambamba na Mkewe Mariam Shamo wakiwa na mmoja wa  wageni wao,Mwamvita Makamba kutoka kampuni ya simu za mikononi ya  Vodacom.
 
 Balozi Shamo na Mkewe wakiwa na wageni wao waalikwa waliofika kujumuika nao kwenye hafla hiyo.
 
 Mke wa Balozi,Mariam Shamo (wa nne shoto) akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa.
 
 Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiwa na Mkewe Juhayna Kusaga wakifurahia jambo kwenye hafla hiyo
 
 Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally  Hassan Mwinyi akizungumza jambo na Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza  kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons).
 
 Rais  mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi akizungumza machache  kuhusiana na hafla hiyo kwa baadhi ya wanahabari waliohudhuria ,shoto ni  Sir Andy Chande.