Pages

Tuesday, July 10, 2012

BABA MZAZI WA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AFARIKI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda amefiwa na baba yake, imefahamika.Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Jenista Mhagama alitoa taarifa hiyo bungeni mchana huu wakati akiahirisha kikao cha asubuhi cha mkutano uliokuwa ukijadili hoja ya bajeti ya Wizara ya Maji.

Mhe. Jenista alisema kuwa Pinda hatakuwepo bungeni kwa vile amekwenda kushughulikia msiba wa baba yake. Akaongeza kuwa kwa sababu ya msiba huo, Waziri Mkuu amemteua Waziri wa Afrika Mashariki, Mhe. Samwel Sitta kuwa mkuu wa shughuli za serikali bungeni kuanzia leo (Julai 10) hadi Julai 15.
--
Viongozi Mbalimbali Walimtembelea Baba Mzazi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Rais Jakaya Kikwete akipokea zawadi ya kuku kutoka Mama Albertina Kasanga ambaye ni Mama mzazi wa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda wakati Rais Kikwete alipowatembelea akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Mpanda, Rukwa. Kushoto ni Mzee Xaveri Kayanza Pinda, Baba yake Waziri Mkuu.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Baba mzazi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Exavery Kayanza Pinda, wakati alipokuwa akipita kuelekea Kijiji cha Mwamapuli akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi Februari 20. 2012. Kulia nia Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Eng. Stella Manyanya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitaniana na Mzee Kayanza Pinda alipokuwa anamuaga kuelekea kwenye mahafali ya Shule ya Sekondari Usevya ambapo alienda kumuwakilisha Waziri Mkuu aliyekuwa amealikwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye mahafali hayo. Miongoni mwa utani alioutoa Mzee Pinda ni pamoja na kumuita Mkuu huyo wa Mkoa "Mnyatomato" kumaanisha kuwa ni Mtoto wa Manyanya ambapo nyanya kwa kiingereza ni Tomato. Hahahahaaah!

Popular Posts