Pages

Friday, November 23, 2012

Dk Emmanuel Nchimbi Kuzindua namba mpya za magari ya Jeshi la Magereza.


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi 
---

DAR ES SALAAM, Tanzania

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi uzinduzi wa namba mpya za magari ya Jeshi la Magereza. kesho kutwa Novemba 24.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari na kusainiwa na Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza (CP), Chamulesile, ilieleza kuwa uzinduzi huo utafanyika kuanzia saa 4:00 asubuhi katika Gereza Kuu la Ukonga jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa uzinduzi huo unazingatia Sheria ya Usalama Barabarani Sura ya 162 iliyofanyiwa marekebisho ya kanuni ya Usalama Barabarani (Amendment, ya 2004).

Taarifa hiyo ilisema kuwa, marekebisho hayo yalitangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na.102 la Machi 23 mwaka huu, na yalitoa nguvu ya kisheria kwa magari ya Jeshi hilo kuanza kutumia namba mpya zenye jina la jeshi hilo la Magereza.

Aidha, magari ya Jeshi la Magereza yatatambulika kirahisi wakati wa kutekeleza majukumu yake.

Popular Posts