Pages

Friday, November 23, 2012

Tume ya Mabadiliko ya Katiba Yakusanya Maoni Tarime,Mara



Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphery Polepole (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa wananchi wa Kata ya Mliiba, Wilaya ya Tarime mkoani Mara wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume hiyo jana alhamisi Nov.22, 2012. Wajumbe wengine wa Tume, wa kwanza kulia Nassor Mohammed, Maria Kashonda na Riziki Ngwali.
Wananchi wa kijiji cha Mangucha Kata ya Nyanungu Wilaya ya Tarime mkoani Mara wakifuatilia mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya uliotishwa na Tume ya Mabadlliko ya Katiba jana  alhamisi Nov. 22, 2012 katika kijiji hicho.
---
Na Ismail Ngayonga-Tarime, Mara

MKAZI wa Kata ya Kata ya Mliiba Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Marco Magubo (31) amependekeza ni vyema Katiba Mpya ikataze vyama vya siasa vinavyoingia madarakani mara baada ya kushinda uchaguzi wa Rais visipeperushe bendera yake na badala yake kuweka bendera ya Taifa.

Akitoa maoni yake jana (Alhamisi Nov. 22, 2012) kuhusu Katiba Mpya kwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alisema kitendo cha kupeperusha bendera ya chama kilichoingia madarakani kitaongeza chuki kwa wanachama wa Chama kingine cha siasa kilichoshindwa uchaguzi.

Aidha Magubo alisema Rais anayeingia madarakani anawakilisha maslahi ya wananchi wote na hivyo si busara kwa Chama kilichoshida uchaguzi kupeperusha bendera ya Chama chao kwani Kiongozi huyo haongozi wanachama wa chama chake pekee bali wananchi wote katika taifa.

“Tazama Marekani ambao hivi majuzi tu walifanya uchaguzi mkuu wa Rais, katika kampeni za vyama vyao hatukuweza kuona bendera ya Republican wala Democracy ambavyo vyote vilishiriki uchaguzi na badala yake tuliona wananchi wakipeperusha bendera ya Taifa lao na hatukuona bendera ya Republican wala Democracy” alisema

Alisema kwa kuwa Tanzania ni nchi ya umoja, amani na mshikamano ni vyema  Katiba Mpya ikewe kipengele cha kukataza bendera za vyama vyao na badala ya wamwachie Kiongozi aliyopo madarakani kutetea hoja za wananchi wote.

Popular Posts