Pages

Friday, November 23, 2012

Katibu Mkuu wa CCM Abdurahamn Kinana Atua Mkoani Rukwa na Kusema'' Kuitwa Waheshimiwa Ndani ya CCM Sasa Basi.''


Katibu Mkuu Mpya wa CCM Abdurahaman Kinana akifungua shina la wakereketwa wa CCM la Kisesa, mkoani Rukwa.
Katibu Mkuu Mpya wa CCM Abdurahamn Kinana,na Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye , na Mzee Self Khatib wakisalimia wananchi Uwanja wa Ndege wa Rukwa.
Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akiwa na Watoto
Katibu Mkuu Mpya wa CCM Abdurahaman Kinana akizungumza na wana-CCM leo mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa
Pikipiki za mapokezi kutoka Uwanja wa Ndege wa Rukwa.Picha na Bashir Nkromo-Rukwa
---
NA BASHIR NKOROMO, RUKWA
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameagiza kuanzia sasa wanachama wa CCM kuacha kuitana waheshimiwa badala wake watumie jina ndugu kama alivyoasisi Mwenyekiti wa kwanza wa CCM, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Kinana ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na viongozi wa CCM, mjini hapa, akiwa katika siku yake ya pili ya ziara ya siku nne kujitambulisha na kukagua uhai wa Chama katika mkoa huo na mikoa ya Mtwara, Geita na Arusha.

"Mimi katika maisha yangu yote ya kumfahamu Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, sikupata kumsikia akijiita au akitaka aitwe Mheshimiwa Mwenyekiti, au Mheshimiwa Rais, sasa haya mambo ya sisi kuitama mheshimiwa tunayatoa wapi?", alihoji Kinana.

Alisema, Mwalimu Nyerere hakujiita Mheshimiwa kwa sababu na maana kubwa sana, kwa hiyo ni lazima Wana-CCM kuendelea utamaduni huo wa kuitaka ndugu kwa sababu unazuia matabaka ya ubwana na utwana.

Mapema kabla ya mkutano huo wa ndani, Kinana alifungua shina la wakereketwa wa CCM Isesa na shina la UWT, Chanji nje kidogo ya mji wa Sumbawanga, ambapo alisema hatua ayake ya kufungua matawi hayo na kushiriki kikao cha shina kinachofunguliwa na mjumbe wa shina husika, ni ishara ya kuwaagiza viongozi wa ngazi zote wa CCM kuhakikisha wanatembelea mashina na matawi.

"Hili siyo langu, ni agizo la Mkutano Mkuu wa CCM uliomaizika mjini Dodoma hivi karibuni, pale tuliazimia kwamba, ili kuimarisha uhai wa Chama lazima viongozi wa ngazi mbalimbali watembelee mashina ma matawi ili kuzijua kero zilizopo huko", alisema.

Alisema, kulingana na agizo hilo, sasa kila kiongozi wa Chama atapimwa ufanisi wake wa kikazi kwa kuangalia ni namna gani anafanya kazi zake kwa karibu sana na mashina na matawi.

Alisema, CCM imesisitiza lifanyike hilo kwa juhudi zaidi kwa sababu ni wazi kwamba wenye chama ni wanachi waliopo kwenye ngazi hizo za mashina na matawi, hivyo kwenda huko ndiko kutaimarisha chama kwa uhakika zaidi.

Katika ziara hiyo, Kinana amefuatana na wajumbe wa NEC, Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi), Mohamed Seif Khatib (Oganaizesheni)na waziri wa TAMISEMI, Aggrey Mwanri.

Mwisho.

Popular Posts