Pages

Friday, October 19, 2012

Amana Bank Yazinduwa Amana Mobile Banking

 ICT, Manager- Delivery Channels (Bi . Bidala Mohammed Mwandugu ) akielezea jinsi ya utumiaji wa huduma ya Amana Mobile Banking..
 Mkuu wa Kitengo cha Bishara Bw. Sudi Marungu - Amana Bank. akizinduwa huduma ya Amana Mobile Banking.
Uzinduzi wa Amana Mobile Banking.
---
 
Serena Hotel - Dar es salaam,
Tarehe : 18  / Oktoba / 2012
Amana Bank, Benki ya kwanza Tanzania inayofuata Sharia kikamilifu, leo tunazindua huduma ya “Amana Mobile”.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha Biashara  (Amana Bank)  Bw. Sudi Marungu alisema Dar es salaam kuwa “ Amana Mobile ni huduma za kibenki kwa kutumia mtandao wa internet na simu zamkononi.”  “Huduma  hii inalenga kuwa rahisishia wateja wetu kufanya miamala nakupata huduma mbalimbali ambazo zinatolewa  na benki yetu kwa  njia ya mtandao.  Lengo la kuanzisha huduma hii nikurahisisha usimamizi wa akaunti zawateja wakati wowote, popote walipo siku saba za wiki.” 
Akizungumzia kwa ufupi juu ya huduma hii Bw. Sudi Marungu alisema,  “ Amana Bank inajivunia kuwa benki ya kwanza kabisa ya Kiislam nchini Tanzania ikiwa na malengo ya kutoa huduma za kibenki za kisasa na za kipekee ambazo zinafuata Sharia kikamilifu kwakuzingatia maadili na kwa njia iliyowazi na kwakutumia teknolojia ya kisasa kwamanufaa ya wateja wetu wote.”
Hata hivyo, alisema  ni kwa kutumia teknolojia hii ya kisasa Amana Bank leo hii inazindua huduma ambayo inaenda sambamba na maendeleo yakiteknolojia duniani. Mteja wa sasa anahitaji kufikiwa na huduma za ki benki popote pale alipo wakati wowote. 
Amana Mobile itapatikana kupitia simu za mkononi na wateja ambao wameunganishwa na mitandao yote ya simu wanaweza kutumia huduma hii. 
Wakati huduma za kibenki kupitia mtandao yaani  “Internet Banking”  zinaweza kufanyika kupitia kompyuta ambazo zimeunganishwa namtandao wa internet. Huduma hizi ni zaharaka na rahisi hivyo humuwezesha mteja kufanya miamala ya kibenki popote alipo kwa wakati anaotaka. Amana Mobile inalenga kutoa huduma mbalimbali za kibenki kupitia simu za mkononi.
Kupitia Amana Mobile wateja wetu wataweza kuuliza salio la akaunti zao, kupata taarifa fupi na taarifa kamili za akaunti zao, Kununua muda wa maongezi kwa mitandao yote ya simu zamkononi, Kufanya malipo ya awali na Ankara kama vile kununua LUKU, kulipa bili za DAWASCO, Star Times, TTCL Broadband, Uhuru one,  DSTV nakadhalika.             Pia Amana Mobile inamuwezesha mteja kuomba kitabu cha hundi, kuhamisha fedha kutoka akaunti moja kwenda nyingine ndani ya benki au kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti yake kwenda kwenye akaunti yake ya simu ya mkononi kama vile M-pesa, TigoPesa na Airtel Money
Kwa upande mwingine Amana Internet Banking inarahisisha usimamizi wa akaunti za wateja wetu kwani wanaweza kufanya miamala yakibenki popote pale walipo duniani..
Moja ya faida kubwa ya huduma hii nikwamba inatoa urahisi wakufanya miamala ya kibenki kwa muda ambao mteja anahitaji huduma hiyo iwe ofisini, nyumbani, safarini au hata akiwa nje ya nchi. Huduma hii imerahisisha miamala midogo midogo ambayo hapo awali iliwalazimu wateja wetu kufika katika matawi yetu kupata huduma sasa kupata huduma popote walipo, kwa urahisi na haraka. 
Hii ni hatua kubwa kwa Amana Bank hasa ikizingatiwa kuwa benki ina miezi kumi tu tangu ilipoanza kutoa huduma kwa wateja. Tunawakaribisha wote kufungua akaunti Amana Bank.
Karibuni katika ulimwengu mpya kabisa wa kibenki, unaofuata Sharia kikamilifu. 
Kwa maelezo na taarifa zaidi unaweza kupata kupitia tovuti  yetu ya www.amanabank.co.tz
Asanteni

Popular Posts