Pages

Friday, October 19, 2012

WILAYA MPYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA MSHINDI WA KWANZA WA SHUGHULI ZA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MWAKA 2012 KANDA YA IV ILIYOSHINDANISHA MIKOA MITANO

Hati kuithibitisha Wilaya ya Kalambo kutoka Mkoa wa Rukwa kuwa mshindi wa kwanza wa shughuli za mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2012 katika kanda ya nne iliyohusisha Mikoa mitano ya Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa na Mbeya na Wilaya zake.
Mkuu wa Wilaya mpya ya Kalambo Moshi Chang'a ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kwenye shughuli za kuzima Mwenge wa Uhuru Mkoani Shinyanga akionyesha Kikombe na Cheti alichokabidhiwa na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama zawadi ya ushindi kwa Wilaya yake baada ya kushika nafasi ya kwanza katika shughuli za mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2012 katika kanda ya nne iliyohusisha Mikoa mitano ya Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa na Mbeya na Wilaya zake alipowasili jana Mkoani Rukwa aikitokea Shinyanga.
 Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akimpa Mkono wa pongezi Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a kwa ushindi alioupata wa Wilaya yake mpya kuwa mshindi wa kwanza wa shughuli za mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2012 katika kanda ya nne iliyohusisha Mikoa mitano ya Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa na Mbeya na Wilaya zake. Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chuma.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa aikifurahia kikombe hicho.
 Ilifanyika tafrija fupi ya kupongezana kwa ushindi huo wa Wilaya ya Kalambo kwani umekuwa ni ushindi wa Mkoa mzima wa Rukwa kutokana na ushirikiano uliopo kutoka ngazi ya Mkoa hadi katika Halmashauri.
 Hakika ushindi huo ulimgusa kila mmoja
 Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ALhaj Salum Mohammed Chima akifurahia kikombe hicho kwa pamoja na watumishi wenzake.
 Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akipokea kikombe hicho cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a muda mfupi baada ya kumpokea akitokea Mkoani Shinyanga alipokwenda kumuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwenye kilele cha kuzima mwenge wa uhuru.
 Watumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa wakifurahia kikombe hicho cha ushindi.
Wawakilishi wa Mkoa wa Rukwa waliokwenda kushiriki kuzima mwenge wa uhuru Mkoani Shinyanga na kurudi na kikombe cha ushindi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a, mratibu wa Mwenge Kimkoa Abubakar Serungwe na Katibu wa Mkuu wa Mkoan Frank Mateny wakipewa mapokezi na uongozi na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.Picha na Habari zimeletwa hapa na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

Popular Posts