Wakati Zanzibar Sakata la Waislamu kuendeleza kitimtim kufuatia kutoonekana kwa Kiongozi wa Kundi la Uamsho Vurugu zimeendelea kutawala eneo la Darajani na kusababisha Polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya watu.
Jijini Dar es Salaam hali si tofauti na hiyo maeneo ya Kariakoo maduka kadhaa yamefungwa kufuatia vurugu kama hizo baada ya Swala ya Ijumaa kufuatia pia kukamatwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda yamekuwa ni matokeo ya vurugu watu kukimbizana huku Polisi wakidhibiti Usalama na Amani kuelekea harijojo.(Picha na Maktaba).
Maeneo ya Posta karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani Askari wameweka utepe wa kudhibiti watu kuingia katika maeneo hayo kitendo kilichosababisha shughuli nyingi kusimama.
Pichani ni Jeshi la Wananchi Tanzania likiwasilia maeneo ya Kariakoo kuongezea nguvu kwa ajili ya kutuliza ghasia. 
Pichani ni Vipeperushi  vilivyotolewa na Waumini wa Dini ya Kiislamu kabla ya maandamano leo

 Picha  juuu Doria kali ya jeshi la polisi ikiendelea jijini Dar es Salaam hivi sasa
 Akari wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)Wakipita maeneo ya kariakooo mchana huu baada ya vurugu kutokea.

 ---
DAR ES SALAAM

Vurugu kubwa zimetokea mchana huu katika maeneo yanayozunguka eneo la Kariakoo na kusababisha hofu kubwa na Polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi na kutawanya mikusanyiko ya watu waliokuwa wamejiandaa kuandaamana kuelekea katika Ikulu ya Magogoni jijini.

Maduka yote katika maeneo hayo yamefungwa na shughuli mbalimbali zimesimama pamoja na Ofisi mbalimbali zimefungwa kutokana na hofu kubwa iliyotanda.