Pages

Tuesday, September 11, 2012

MAANDAMANO YA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Nevile Meena akihutubia katika mkutano uliofanyika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam jana, kulaani ktendo cha Polisi kumuua kwa bomu Mwandishi wa habari wa Kituoc ha Televisheni cha Channel Ten, Mkoa wa Iringa, marehemu Daudi Mwangosi katika vurumai zilizotokea wakati Chadema wakifungua tawi katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi hivi karibuni.
Huyu ni Manyerere Jackton na bango lake
Hili ni moja ya mabango waliyokuwa nayo waandishi
Jese Kwayi, Mzee Maro na mwezake wakiwa kwenye maandamano hayo
" Dk. Nchimbi ondokaaaaa" mwandishi akipaza sauti kuungana na wenzake waliokuwa wanamkataa kuwepo Kwa waziri wa mambo ya ndani Dk Emmanuel Nchimbi
Mwandishi Lauden Mwambona akiwa amefunga mdomo kama hivi wakati wa maandamano hayo
Hawa nao wakati mmoja ameziba mdomo, mwenzake akaziba macho kufikisha ujumbe wa kulaani mauaji ya Mwangosi
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi akiingia kwenye mkutano wa wanahabari viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam leo, walioandamana kupinga mauaji ya mwandishi mwenzao, Daudi Mwangosi wa Channel Ten Tv,
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk.Emmanuarl Nchimbi akajaribu kuwatuliza... waandishi bila mafanikio amabao walimtaka aondoke haraka enepo hilo
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk.Emmanuarl Nchimbi akiondoka akisindikizwa na viongozi wa Jujwaa la Wahariri
Waandishi wakiingia viwanja vya Jangwani.Picha zote na Mdau Richard Mwaikenda na Bashir Nkromo

Popular Posts