
-- 
1.Uwajibikaji  wa kisiasa wa viongozi  wa serikali na idara zake.,Waziri Emmanuel  Nchimbi,IGP Mwema,Paul  Chagonja,RPC Morogoro na Kamanda wa FFU,na RPC  IRINGA na Kamanda wa FFU  wajiuzulu na au wafukuzwe kazi
2.RPC Morogoro na Iringa,makamanda wa FFU Morogoro na Iringa,na maaskari waliouwa wakamatwe mara moja na kufunguliwa mashitaka
3.Rais  aunde tume huru ya  uchunguzi wa vifo tata katika matukio ya  kisiasa.1.ARUSHA vifo  3.IGUNGA,vifo vingi havijulikani bado,3.ARUMERU  MASHARIKI,vifo 5,  4.SINGIDA kifo 1, MOROGORO na IRINGA
chadema haitatambua wala kushirikiana na kamati batili ya NCHIMBI.
4.Msajili  wa vyama vya siasa  John Tendwa ni mtu hatari kwa taifa kwa kauli tata   anazozitoa.anashirikiana na au anajipendekeza kwa CCM na Serikali   yake.CHADEMA tangu sasa haitafanya kazi na Tendwa wala kufanya   mawasiliano naye ya kiofisi.Labda kama atagundua makosa yake na kuomba   msamaha,chadema itatafakari namna ya kufanya naye kazi tena.
5.TBC  TAIFA Television na Redio  ni hatari kwa taifa,kwa kubobea kupotosha  umma juu ya matukio  mengi.Hivyo CHADEMA Inatangaza mgogoro na TBC na  inaelekeza na kuomba  wanachama ,wapenzi,na wananchi wote wapendao  ukweli na haki,kuisusia TBC
6.Jeshi  la Polisi lijue kuwa  Maandamano ndiyo siasa yenyewe na mikutano ya  hadhara ni lazima kwa  mawasiliano ya umma na siasa.kuzuia vitu hivyo ni  kunyima wananchi haki  yao ya kikatiba ya uhuru wa kukusanyika na kutoa  maoni,pia kupata habari  na taarifa
7.Operesheni  MOVEMENT FOR CHANGE  M4C,Inaendelea kadiri ya ratiba ilivyopangwa  katika utaratibu uleule  uliokuwepo awali.Inarejea Iringa Siku si  nyingi.Na kamati kuu Imetoa  msisitizo MAALUM kwa jimbo mojawapo  singida,ambapo wamesema watatumia  helcopita,magari,pikipiki na baiskeli  na miguu,na badala ya kupita  vijijini kama majimbo mengine,Chadema  wanasema kwa sababu maalum katika  jimbo hilo watapita kitongojikwa  kitongoji,ili kufunza adabu baadhi ya  viongozi (msisitizo ni wa msoma  MAAZIMIO.jimbo hili laweza kuwa la  Mwigullu Mchemba,kadiri ya  wanahabari waliokuwepo)
8.Kutokana  na mgogoro wa muda  mrefu mkoani mwanza uliosababisha meye wa chadema  kuvuliwa umeya kinyume  na utaratibu na kwa njama za CCM na Serikali,na  bahati mbaya sana kwa  kushirikisha madiwani wa CHADEMA,KAMATI KUU  imewavua UANACHAMA madiwani  wake wawli 1 ADAMU CHAGULANI wa kata ya  IGOMA na HENRY MATATA wa  KITANGIRI, PIA uongozi wote wa CHADEMA mkoa wa  mwanza Umevunjwa.
Imesomwa na 
Mwenyekiti CHADEMA Taifa