
Msimamizi  wa Kituo cha Afya cha Kendwa Nungwi Bwana Viola Franco kutoka  Hoteli  ya Kimataifa ya Lagema Nungwi inayosimamia Kituo hicho  akimkaribisha  Balozi SeifAli Iddi wakati alipofanya ziara ya  kukitembelea Kituo hicho  kipya kuona hudumazinazotolewa 

Muuguzi  Mkuu wa Hospitali ya Kivunge Dr. Ashura Shaib Mussa  akimuelezea  majukumu yao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif   alipoitembelea Hospitalihiyo iliyopo Wilaya ya Kaskazini A.

    Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Jamal Adam akimuelezea   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif changamoto wanazopambana   nazo Hospitalini hapo ikiwemo idadi kubwa ya wagonjwa.

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi akiwafariji   wazazi Hawa Mashauri na Fatma Mohd waliojifungua katika wodi ya Wazazi   ya Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja alipofanya ziara ya awamu ya pili katika   taasisi za Wizara ya Afya Zanzibar.
--
  Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar umeagizwa kuandaa Mpango Maalum kwa   ajili ya ujenzi wa Hospitali kubwa ndani ya Wilaya ya Kati  itakayosaidia  kuipunguzia msongamano mkubwa wa Wagonjwa   Hospitali Kuu  ya Mnazi  Mmoja.
  Agizo hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif   Ali Iddi alipokuwa akiendelea na awamu ya pili ya ziara yake ndani   yaTaasisi za Wizara ya Afya hapa Zanzibar.
  Balozi Seif aliueleza Uongozi wa Wizara hiyo ya Afya kwamba Serikali  Kuu  itakuwa tayari kuangalia uwezekano wa uwezeshaji wa ujenziwa  Hospitali  hiyo muhimu kwa Jamii.
  “ Tumefikia wakati kulingana na mahitaji ya huduma za Afya kwa wananchi   wetu kuwa na Hospitali kubwa katika kila Wilaya  na hii kwa kiasi   kikubwa itaondosha vurumai isiyo ya lazima katika Hospitali yetu ya   Rufaa ya Mnazi Mmoja”. Alisisitiza Balozi Seif.
  Balozi Seif alisema katika kukabiliana na  changamoto zinazoikabili   Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ameahidi kusaidia Vitanda 10 kwa ajili ya   wodi ya Wazazi na Serikali itajitahidi kutafuta mbinu za kutatuta   changamoto chengine zilizopo.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi   aliwapongezaWatendaji wa Hospitali hiyo kwa utendaji wao wa  kazi licha   ya mazingira magumu wanayofanyia kazi.
  Balozi Seif alishuhudia idadi kubwa ya Wagonjwa wanaopata huduma katika   Hospitali hiyo ambapo Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr.   Jamal Adam  alieleza kwamba uwezo wa kuhudumia wagonjwa bado ni ule ule   tokea miaka ya thamanini wakati idadi ya wagonjwa imeongezeka mara  dufu.
  Akiitembelea Hospitali ya Wazazi ya Muembe Ladu BaloziSeif alielezwa na   Watendaji wa Hospitali hiyo mfumo mpya ulioanzishwa wa makuz iya mtoto   kwa yule aliyezaliwa akiwa pungufu wa uzito ujuilikanayo kwa jina la   Kangaroo.
  Mafunzo hayo tayari yameshaanza kufundishwa kwa Wazazi mbali mbali kwa   lengo la kujiweka tayari endapo Mzazi atatokezewa kujifungua Mtoto   mpungufu.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikagua utendaji wa   wafanyakazi wa Hospitali ya Kivunge ambapo Muuguzi mkuu wa Hospitali   hiyo Dr.Ashura Shaib Mussa alishauri kuwepo kwa Kitengo cha Upasuaji ili   kuwapunguzia hatari wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ya ghafla.
  Dr. Ashura alisema ipo hatari na inaweza  kusababisha kifo kwa mzazi   anayehitaji operesheni ya ghafla kwa kumsafirisha katika masafa marefu   kupatiwa hudumahiyo.
  Akizungumza na Watendaji hao Balozi Seif aliwapongeza Madaktari,  Wauguzi  pamoja na Wafanyakazi wote wa Hospitali ya Kivunge kwajuhudi  zao za  kuiwekea mazingira safiHospitali hiyo.
  Balozi Seif aliahidi kuipatia Hospitali hiyo Vitanda kumi na kuwataka   wajenge utamaduni wa kuvifanyia majaribio Vifaa vipya wanavyopelekewa   hata kama itakuwa bado kuvifanyia kazi pamoja na kuyapatia changa moto   matatizo yanayowakabili.
  “Kama sijajua matatizo na changamoto zilizomo ndani ya Mawiza na  Taasisi  za Serikali wakati mimi ndie Mtendaji Mkuu wa Serikali  nitashindwa  kutoa maamuzi au ufafanuzi pale unapohitajika”. Alisema  Balozi Seif.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimalizia ziara yake kwa kukaguwa   Hospitali mpya ya Wazazi iliyopo katika Kijiji cha Kendwa ambayo   imefadhiliwa na Uongozi wa Hoteli ya Kimataifa ya Lagema. Daktali Mkuu   wa Hospitali hiyo iitwayo R.G.F Matenity Clinic Dr. Hawa Kivembele   alimueleza Balozi Seif kwamba huduma za Hospitali hiyo ambazo ni bure   zilizoanza mapema mwezi huu zimelengwa kwa wanakijiji wa eneo hilo.
  Hata hivyo Dr. Hawa alisema mbali ya wanakijiji haolakini pia Hospitali   hiyo hutoa huduma ya malipo kwa Wafanyakazi wa Hoteli zotezilizoko   katika ukanda huo
Na
 Othman Khamis Ame, 
Ofisi ya  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar