
  Diwani wa Kata ya Kwadelo wilaya ya  Kondoa mkoani  Dodoma, Alhaj, Omary Kariati akiendesha trekta wakati akiwasili kwenye  hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji katika  kata hiyo, jana. Jumla ya sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3,  alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki  zilipatikana pamoja na gunia 37 za alizeti yenye thamani ya sh.  35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Kushoto ni Mwenyekiti wa  wakulima wa Kwadelo, Sheikh Khamis Nchallo. .
 
  Trekta  64 za wakulima wa Kata ya Kwadelo, Kondoa  mkoani Dodoma, ambazo wamezipata kwa jitihada za diwani wa kata hiyo,  Omary Kariati kutoka Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa- SUMA  JKT, zikiwa zimeegeshwa eneo la mkutano ulioitishwa na diwani huyo, kwa  ajili ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa  maji wa kata hiyo, jana. Wakulima hao walifika na trekta hizo na kuwa  mstari wa mbele kuchangia mradi huo wa maji.  Jumla ya sh. milioni 4.5,  zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii,  Balozi Khamis Kagasheki  zilipatikana pamoja na gunia 37 za  alizeti yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi  zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Bernard Membe.
 
 Wakazi wa  Kata ya Kwadelo, wilaya ya Kondoa  mkoani Dodoma, wanakabiliwa na uhaba wa maji safi na salama kwa zaidi ya  miaka 20 sasa, kutokana na miundombinu iliyozinduliwa mwaka 1973, na  Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere,  wakati wa uhai wake,   kufa kwa kukosa uangalizi. Pichani Diwani wa Kata hiyo, Omary Kariati  (wapili kulia) na Msaidizi wake  Bakari Ndee wakionyesha tangi la maji  lililozinduliwa na Baba wa Taifa ambalo sasa halifanyi kazi.  Diwani alionyesha tangi hilo,  wakati wa harambee ya kuchangisha fedha  za kufufua mradi wa maji. Sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3,  alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki  zilipatikana. Pia gunia 37 za alizeti zenye thamani ya sh. 35,000 kila  moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe zilichangwa kwa ajili hiyo.  Kulia ni Mwenyekiti wa wakulima wa Kwadelo, Sheikh Khamis Nchallo. 
 
    Mkazi wa Kijiji cha Makirinyi, Khadija Mussa,  akikabidhi  kiroba cha alizeti kwa diwani wa Kata ya Kwadelo, Wilaya ya  Kondoa mkoani Dodoma, Omary Kariati kuchangia ujenzi wa zahanati ya  Kijiji hicho, wakati wa harambee ya kutafuta fedha za ujenzi wa  zahanati, uliondeshwa na diwani huyo, jana. Jumla ya magunia 17 yenye  thamani ya sh. 35,000 kila moja, na sh. milioni 9.2 vilipatikana, ikiwa  ni pamoja na sh. milioni 7 zilizochangwa na  Waziri wa Maliasili na  Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
 
  Diwani  wa Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani  Dodoma, Alhaj, Omary Kariati, akionyesha mtaro ulichimbwa na Baba wa  Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati wa uhai wake mwaka 1973, kwa  ajili ya mradi wa maji katika Kata ya Kwadelo, Wilaya ya Kondoa mkoani  Dodoma, jana. Hata hivyo mradi huo ambao ulikuwa ukihudumia watu 1,200  wakati huo, umekufa miaka 20 iliyopita na  sasa diwani huyo anaunganisha  nguvu za pamoja za wananchi na serikali ya CCM kuufufua. Kwadelo sasa  ina watu 11,800.
 
 Msichana  katika kijiji cha Kwadelo, Wilaya ya  Kondoa mkoani Dodoma akitumia baiskeli kutafuta maji, katika kijiji cha  Makiranya, jana.
 
 Wazee wa  Kata ya Kwadelo, wakipungua mikono  kumuaga Diwani wa Kata hiyo, Omary Kariati, alipokuwa anaondoka baada ya  kuendesha harambee kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufuma mradi wa  maji, jana.Picha na Bashir Nkromo