Pages

Friday, August 31, 2012

KAMANDA UVCCM IRINGA AWAPA SOMO VIJANA IRINGA VIJIJINI

kamanda wa UVCCM wilaya ya Iringa vijijini Arif Abri akifungua mkutano wa uchaguzi wa UVCCM wilaya ya Iringa vijijini leo
Wajumbe wakiwa wamependeza kwa sare zilizotolewa na kamanda huyo na mbunge Lukuvi na Mgimwa
Waandishi wakipewa kadi za CCM Leo


CHANGAMOTO imetolewa kwa vijana wa Chama cha mapinduzi ( UVCCM) wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa kufanya kazi kwa kujituma zaidi badala ya kuendelea kulalamika vijiweni bila kufanya kazi.

Changamoto hiyo imetolewa Leo katika ukumbi wa Sekondari ya Mwembetogwa mjini Iringa na mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa UVCCM ambaye pia ni kamanda wa UVCCM wilaya ya Iringa vijijini Arif Abri .

Abri amesema kuwa hivi sasa imejitokeza tabia ya vijana kulalamika juu ya hali ngumu ya maisha hata kuhoji juu ya maisha bora huku sehemu kubwa ya vijana hao wakiendelea kushinda vijiweni jambo ambalo ni kinyume na harakati za kujitafutia maisha bora kwa kila mtanzania.

Hata hivyo amewataka vijana hao kuendelea kujishuguulisha na shughuli za Uzalishaji mali ikiwa ni pamoja na kujiunga katika vikundi vya kiuchumi ili kuiwezesha serikali kuweza kuwasaidia mikopo yenye masharti nafuu.

Abri amesema kuwa vijana ambao ni tegemeo kubwa katika Taifa bado wanalojukumu kubwa la kuendelea kuwavuta vijana wenzao ambao wanakimbilia vyama vya upinzani.

wakati huo huo Abri amewapongeza wanahabari watano mkoani Iringa ambao wamejiunga na UVCCM wilaya ya Iringa vijijini.

Katibu wa UVCCM wilaya ya Iringa vijijini Frank Kibiki aliwataja wanahabari walioniunga na CCM kuwa ni meneja wa IT Ebony Fm Eliud Kalokola , Flora Kamaghe kutoka gazeti la Uhuru, Zuhura Zukheli kutoka radio Qibra ten ,Wiliam Muro kutoka gazeti la kwanza jamii na NEEMA Mgulanga mwanahabari wa kujitegemea .

MWISHO

Popular Posts