
 Ommy Dimpoz akipagawisha mashabiki wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma, katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
 
 Mmoja  wa wasanii waliyoibuka kidedea katika mchakato wa Serengeti Super Nyota  2012, akidhihirisha uwezo wake wa kuimba ndani ya uwanja wa Karume  mjini Musoma.
 
 Mwasiti  akiwa amepakatwa na mmoja wa mashabiki zake kwenye Tamasha la Serengeti  Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma huku akiyamwaga  mauno ya kiuchokozi chokozi.
 Bofya hiyo video uone jinsi palivyokuwa  hapatoshi ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma,wakati tamasha la  Serengeti Fiesta 2012 lilipokuwa linaunguruma usiku wa kuamkia leo.
   Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Roma  Mkatoriki, akiwajibika mbele ya mashabiki wake, kwenye jukwaa la  Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma usiku wa  kuamkia leo.
 
 Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Farid  Kubanda a.k.a Ngosha the Swagadon, akiwaimbisha mashabiki (hawapo  pichani) wake waliokuwa wamefurika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta  2012, ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
 
  Msanii wa filamu Bongo, Vincent Kigos  'Ray',akionesha manjonjo yake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,  muda mfupi baada ya kukaribishwa kwa ajili ya kuwasalimia baadhi ya  mashabiki zao waliokuwa wamefurika ndani ya uwanja wa Karume mjini  Musoma.
 
  Wasanii wa Filamu Steve Nyerere  (kushoto), na Aunt Ezekiel wakishindana kuonesha uwezo wa kuzungusha  mauno yao katika tamasha la Sererengeti Fiesta 2012, lililofanyika  kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma. 
 
  Sehemu ya umati uliyofurika viwanjani  hapo ukifuatilia kwa makini makamuzi ya wasanii hao wa Filamu, kwenye  Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
 
  Msanii mwenye umbo kubwa katika tasnia  ya filamu Bongo, Jacob Steven 'JB', akionesha uwezo wa kunengua kwenye  Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja vya Karume mjini  Musoma. 
 
  Kati ya mashabiki waliyoshindwa  kujizuia katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012, wakizungusha nyonga  zao kama inavyoonekana kwenye viwanja vya Karume mjini Musoma. 
 
  Ray na Steve Nyerere (wa kwanza kutoka  kushoto), wakishindana kusakata sebene kwenye Tamasha la Serengeti  Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
 
 Ray akipagawa na jukwaa huku makelele yakiwa yametawala kila kona uwanjani hapo.
 
 Rais wa masharobaro Bongo, Bob Junior  (katikati), akisongesha burudani za Serengeti Fiesta 2012, na Wanenguaji  wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
 
 Mkongwe  wa muziki wa Bongo Fleva Profesa Jay akionesha uwezo wake wa kukamua  jukwaani kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa  Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
 
 Dimpoz na wanenguaji wake, wakiwajibika kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya viwanja vya Karume mjini Musoma.
 
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo  Rachel (kushoto), akionyesha uwezo wake katika uwanja wa Karume mjini  Musoma, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 na wanenguaji wake. 
 
 Rachel akikamua kwenye uwanja vya Karume mjini Musoma ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012. 
 
 Chege,Temba na Bi Cheka wakiwajibika jukwaani kwenye onesho la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
 
 Mashabiki wa kizungu wakipagawa na burudani ya Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini msoma.
 
 Baadhi ya sehemu ya umati wa mashabiki waliozama ndani ya viwanja hivyo wakishuhudia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.
 
 Msanii wa michano ya Bongo Fleva, Nay wa Mitego akipagawisha jukwaani kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
 
 Mmoja wa Ma'DJ wa Clouds TV, PQ akisababisha burudani ya Serengeti Fiesta 2012 mjini Musoma.
 
 Mashabiki wa burudani za Serengeti Fiesta 2012, wakiwa wamefurika uwanjani hapo tayari kwa kushuhudia burudani mbalimbali.
 