Mwendesha Pikipiki wa Kinondoni, Msawila Mahonda, akionyesha  uwezo wake wa kuchezea Pikipiki, wakati wa mazoezi yao ya kila siku ya  Jumapili kwenye Viwanja vya Tanganyika Pakers, Kawe jijini Dar es  Salaam. 
Pamoja na waendesha Pikipiki hao kujitahidi  kutengeneza njia na uwanja wa mchezo huo katika eneo hilo kwa kujitolea  na kuwafanya mashabiki lukuki wa mchezo huo kukusanyika kila siku ya  jumapili ili kupata burudani, lakini bado mchezo huo haupewi 'Sapoti' ya  kutosha na wadau wa michezo nchini na Wizara husika kama ambavyo  inaonekana katika michezo mingine kama ulivyo chezo wa Soka ambao kila  kukicha wanajitokeza wadhamini wa mchezo huo na kumwaga 'Mihela' mingi  kwa kupromoti jambo ambalo tayari limekwishapita katika hatua hiyo  likisubiri hatua nyingine. 
Picha inayofuata ni mwendesha Pikipiki wa  nje.
 Kwa wenzetu wanaojua nini maana ya michezo huandaa kama hivi,  njia za pikipiki njia nzima ikia na alama za kuwaongoza madereva pindi  wanapokuwa mchezoni.
 Kwa wenzetu hata uwanja unakuwa umeandaliwa kama hivi, na wale  wanaopenda michezo hujitangaza kupitia mchezo huo kama inavyoonekana  pichani mabango kibao ya matangazo.
 Hapa mpiga picha aliyepiga picha hii hakukusudia kupata shoti  iliyobora tu ya mwendesha pikipiki huyu, bali alikusudia na 'Back  Ground' ya watu na matangazo yanayoonekana picha kuashiria mvuto wa  mchezo huu.
 Hata picha ikipigwa kwa mbali lakini bado kilichopo uwanjani  hapo hakiongopi kitaonekana tu kuwa ni mashabiki lukuki wa mchezo huu na  matangazo ya biashara.
 Kwenye Uwanja wetu wa Tanganyika Parkers Kawe kamwe hutamkuta  Rider akicheza kama hivi, si kama hawawezi la hasha ila mazingira ya  uwanja hayaruhusu, ''tuwasapoti ili tuone uwezo wao''
 Hebu ona hizi njia zilivyoandaliwa. Sidhani kama kweli hawapo  wadau wenye uwezo wa kujitolea kufanya kama hivi ili kuuendeleza mchezo  huu.
 Rider, anafanya atakavyo kutokana na kuandaliwa kwa njia nzuri.
 Si kwamba Pikipiki inamuendesha, hapana yeye ndiye anaiendesha  Pikipiki, yote haya yanawezekana tukiwa na nia na pia tutawavutia hata  majirani zetu, kama imewezekana kujengwa Uwanja wa Soka wa kisasa  itashindikanaje Uwanja wa mchezo huu pendwa?.
 Hizi zote ni burudani hadi wewe mshabiki unavutiwa kufika ili  kujionea live, kama ilivyo kwa Kawe lakini haipatikani raha kamili  kutokana na ubovu wa maeneo.
 Action hii na tangazo lililo nyuma ya picha hii unazani Kampuni  hii imejitangaza kwa kiasi gani?.
 Hebu ona njia hizi chini (kulia).....
 Kutokana na kuandaliwa kwa njia kama hivi ndiyo siri ya Rider  huyu anayeonekana yu hewani zaidi.
 Yote haya ni machejo tu, hapa chini yake ndipo ilipo njia yenye  tuta kubwa.
 Haya anaweza kuyafanya Rider Mbongo maarufu kama Ludan Volvo,  akiwezeshwa.
Hebu sasa tujionee viwanja vyetu vya Kawe pamoja na mashine  wanazotumia Marider wetu.
 Huyu ni Msawila akiruka tuta...Kawe Dar es Salaam.
 Marider, Dotto (nyuma) na Msawila, wakichuana wakati wa  mazoeziyao Kawe...
 Mchuano wa Dotto na Msawila unaendelea......
 Mchuano unaendea.......
 Hapa wote wakilala lwenye kona ambayo haina alama yeyote na  pembeni kama inavyoonekana pembeni ikiwa imeegeshwa Pikipiki  isiyohusiana na mchezo huo jambo ambalo ni hatari.
 Rashidi Kiparacha, akiruka tuta....
 Rashidi Kiparacha akiendelea kujifua....
 Kutokana na ubovu wa uwanja huo usio na maandalizi ya kutosha  umesababisha Rashid Kiparacha kujikuta akiuvaa msitu huu wenye miba  baada ya pikipiki yake kugoma ghafla kushika breki.
Makofia akionyesha uwezo wa kupita katika  mabonde.

























