Waziri  wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud   akielezea jambo kwa Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God   Zanzibar Dickson D,Kaganga wakwanza kulia kuhusiana na kuchomwa moto kwa   Kanisa hilo liliopo Kariakoo Mjini Zanzibar katikati ni  Mkuu wa Jeshi   la Polisi I,G,P Saidi Mwemwa.
 Mku  wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwema akitoa hotuba kwa Maaskofu na   baadhi ya waumini wa Kikristo katika kanisa la Tanzania Assemblies of   God Zanzibar lililochomwa moto,ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na   baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.kuliani kwake ni Mkuu wa Mkoa wa   Mjini Abdalla Mwinyi na kushoto yake ni Kamishna wa Jeshi la Polisi   Zanzibar Mussa Ali Mussa.
 Mkuu  wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Abdalla Mwinyi Khamis akitoa   hotuba na kuonyesha Umoja na Mshikamano uliokuwepo kati ya Waislam na   Wakristo kwa Picha ambayo imebuniwa na Mchoraji wa kingereza na kuwataka   kuendelea na mshikamano wao ili kuzidi kuleta amani nchini.
 Askofu  wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson  D,Kaganga  akielezea  kwa Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa  Rais wa  Zanzibar Mohd Aboud na Viongozi wengine mbalimbali kile  kilichotokea  baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea  Zanzibar  ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa  na tokeo  hilo.
 Askofu  wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson  D,Kaganga  akibubujikwa na Machozi kwa kuguswa na hotuba iliokuwa  ikitolewa na  Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Mohd Aboud  baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea  Zanzibar  ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa  na tukio  hilo.
 Mkuu  wa Dini ya Kiislam Afisi ya Mufti wa Zanzibar Thabit Noman  Jongo  akitoa hotuba ya Dini inavyoeleza kuhusiana na kudumisha Amani na   Usalama katika nchi na kuondosha mifarakano na chuki na kuharibu   mali.Katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar ambalo   limechomwa moto.  
Askofu  wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson  D,Kaganga  akimuonesha Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais  Mohd Aboud  maeneo yalioathirika zaidi baada ya Kanisa hilo kuchomwa moto  katika  Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30  wamekamatwa  na  baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.Picha na Yussuf Simai-Zanzibar