Kwa Madaktari wote
YAH: KUAHIRISHWA KWA MKUTANO WA MADAKTARI WOTE NCHINI
Chama  cha madaktari Tanzania (MAT) na Kamati ya Jumuiya ya Madaktari nchini  tunapenda kuwataarifu madaktari wote kuwa ule mkutano wa mrejesho wa  mazungumzo ya kamati ya Rais ya kushughulikia mgogoro wa madaktari na  serikali uliopangwa kufanyika jumamosi tarehe 2/6/2012 umeahirishwa hadi  jumamosi tarehe 9/6/2012.
Hii ni kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kukamilika kwa taarifa ya  kikao cha leo (cha kamati ya rais) (31/05/2012), pia kamati inaendelea  kukusanya taarifa muhimu kuhusu msimamo wa mwisho wa serikali katika  madai yetu yote ili tuweze kuwa na mrejesho uliokamilika.
Madaktari wote tunaombwa kuhamasishana na kuhudhuria kwa wingi kikao  hicho cha tarehe 9/6/2012 kwani kitakuwa kikao muhimu sana kwa  mustakabali wa fani yetu, huduma kwa wagonjwa na maisha yetu.
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza
Dr. Namala P. Mkopi
MAT, President 
                      -