Pages

Sunday, July 15, 2012

DAVID HAYE AMCHAKAZA CHISORA AMCHAPA KWA KO

Bondia David Haye (kushoto) akimpeleka chini, Dereck Chisora, baada ya kumaliza pambano hilo kwa KO katika raundi ya tano katika pambano lao lililopigwa jana usiku.
*****************************************
BINGWA wa zamani wa dunia uzito wa juu, David Haye, amemaliza kazi kwa kumfunga mdomo mpinzani wake Chisora, baada ya kumchapa katika raundi ya tano ya mchezo huo uliokuwa na msisimko mkubwa kutokana na wapinzani hao kutambiana na kutishiana kuchapana wakati wakipima utizo juzi.

Pambano hilo lililosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa masumbwi na hasa kutokana na kuchelwa kutokana na utata wa vibali wa mabondia hao waliokuwa wamefungiwa kupigana na mamlaka za ngumi.

Katika pambano hilo, Haye, alionekana kutawala pambano hilo kwa kuanza kwa kasi ya ajabu tangu mwanzo wa raundi ya kwanza huku akionekana kujiamini zaidi na kumfanya Chisora kushindwa kabisa kujibu mashambulizi hadi ilipofika raundi ya tatu alipofanikiwa kurusha ngumi ya kwanza na ya maana usoni mwa Haye.

Chisora ambaye kabla ya pambano hilo, alikuwa akijigamba zaidi kwa tambo nyingi akidai kumchapa Haye na kwamba ataingia katika pambano hilo kama 'kichaa' na kuweka ahadi kuwa angemdondosha Haye katika raundi ya saba.

usemi wake huo ulikuwa ni kinyume kwani yeye ndiye aliyeweza kupelekwa chini mara mbili katika raundi ya tano na mchezo huo ukamalizika katika raundi hiyo ya tano baada ya kuhesabiwa na kusimama lakini akionekana kushindwa kuendelea na pambano hilo.

Muda mfupi baada ya kuruhusiwa kuendelea na pambano, Haye hakutaka kumpa muda wa kurejea katika hali yake ya kawaida, akamfuata haraka na kuendelea kushambulia. Ngumi tano mfululizo zilizoingia kwenye taya na usoni zilimpeleka chini Chisora ambaye wakati akijaribu kuinuka, refa alimaliza pambano.

Kwa ushindi huo, Haye aliongeza rekodi ya mapambano yake kuwa ameshinda 26 (24 kwa KO) na amepigwa mawili hajatoka sare, wakati Chisora sasa amepigwa mara 4, ameshinda 15 (9 kwa KO) na hajatoka sare.
Chisora akipokea konde zito la taya la kushoto kutoka kwa Haye.

Popular Posts