
   Ministry Kagasheki, Dk Aloyce Nzuki and  Mussa Ibahim  walk across the  pitch at Century Link Field in Seattle, Washington with the massive  Tanzania advertising in the background
 
    The  Delegation from the Ministry of  Natural Resources and Tourism & The Seattle Sounders FC meet at the  Sounders Training Facility Veronica Ufunguo - Tourism Manager -  Ngorongoro Shaun Angell - Account Executive, Seattle Sounders FC/Seattle  SeahawksDr. Aloyce K. Nzuki - Managing Director Tanzania Tourism  BoardTaylor Graham - Manager of Business Operations, Seattle Sounders  FCLuke Grothkopp - Director, Partnership Development, Seattle Sounders  FC/Seattle SeahawksHonorable Ambassador Khamis Kagasheki - Minister for  Natural Resources and TourismRon  Jenkins - Vice President, Corporate Sponsorships - Seattle Sounders FC /  Seattle Seahawks Egidius Mweyunge - Assistant to Minister  KagashekiIbrahim Mussa - Director of Tourism - Ministry of Natural  Resources and Tourism Johnson Manase - Tourism Manager - TANAPADeo  Malogo - Tourism Manager 
  --
  Na Mwandishi Wetu, Renton, Washington.Timu ya Seattle Sounders FC imetangaza ushirikiano na Tanzania, nchi ambayo ni nchi kubwa kabisa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.Ushirikiano huo ulitiwa saini na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Balozi Hamis Kagasheki (Mbunge) na Mmiliki wa timu ya Seattle Sounders Joe Roth katika hafla fupi iliyofanyika jana mjini Renton.
Mbali ya Waziri Kagasheki, wengine walioshuhudia kutiwa saini kwa ushirikiano huo ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mheshimiwa Balozi Mwanaidi S. Maajar, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania Dr. Aloyce Nzuki na maofisa wengine kutoka Wizara ya Utalii, Ubalozini na maofisa wa Seattle Sounders FC. Mambo muhimu katika ushirikiano huo ni uwekwaji wa alama za vivutio vya utalii vya Tanzania katika maeneo mbali mbali kama CenturyLink Field na Starfire Sports Complex, uwanja wa mazoezi wa Sounders FC uliopo eneo la Tukwila.
Vivutio mbali mbali vya Utalii wa Tanzania vitawekwa katika maeneo hayo kama picha za Mlima Kilimanjaro, Hifadhi za Serengeti, Ngorongoro Crater na Zanzibar.
"Ushirikiano wetu na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) utasaidia kutangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania nje ya mipaka yake kwani kuna vivutio vya ajabu mno na kuleta unafuu kwa watalii ,” alisema Mmiliki wa timu ya Sounders FC, Joe Roth. Na kuongeza kuwa ushirikiano huo utatoa nafasi muhimu kwa soko la Utalii wa Tanzania nchi ya mipaka yake.
Waziri Kagasheki mbali ya kupongeza kwa kufanikisha hatua hiyo muhimu katika sekta ya Utalii nchini alisema kuwa ushirikiano huo utatoa fursa nyingi kwa Watanzania na Wamerekani kwani utahimarisha juhudi za Wizara ya Utalii katika kukuza soko la Utalii wa Kimataifa na wa Ndani.
Mheshimiwa Kagasheki pia alisema kuwa ushirikiano huo utatoa fursa za kibiashara kwa nchi zote mbili na kuongeza uwekezaji.