Makamu  Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt.Amani Abeid Karume,  akiendesha kikao cha kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya  Zanzibar, leo katika ukumbi wa CCMKisiwandui Mjini Zanzibar, (kushoto)  ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, pia Mjumbe wa  Kamati Kuu ya CCM Taifa Dkt. Ali Mohamed Shein. Picha na Ramadhan  Othman,Ikulu
 Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati  Kuu ya CCM Taifa Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa  CCM, alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini  Zanzibar, kushiriki katika kikao cha siku moja cha Kamati maalum ya  Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar, kilichofanyika leo. 
Wajumbe  wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar,wakiwa katika kikao  cha siku moja chini ya Mwenyekiti wake, Makamu Mwenyekiti wa CCM  Zanzibar na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume,wakiwa   katika ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar, leo.


