Pages

Monday, August 13, 2012

SIKU YA KIMATAIFA YA VIJANA DUNIANI

Kikundi cha Sarakasi cha Rayon Kids kutoka Temeke kikitoa burudani wakati wa maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel (katikati) kwa niaba ya Waziri Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara katika meza kuu wakati wa maadhimisho ya siku ya Vijana Kimataifa Duniani ambapo Tanzania iliadhimishwa katika viwanja vya Temeke Mwembeyanga. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Bi. Mariam Khan na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la AMREF Bw. Festus Ilako.
Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Bi. Mariam Khan (kushoto) akisalimia umati wa wakazi wa jijini Dar (hawapo pichani) na kutoa ujumbe kwa vijana kuungana na kujiepusha na mangonjwa hatarishi. Kulia Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Bi. Mariam Khan.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel akiwasilisha ujumbe kwa niaba ya Waziri wa Wizara ya Vijana Utamaduni na Michezo ambapo amewataka vijana kujitambua na kuwa na mikakati endelevu na kukaa kama vikundi ili Serikali iweze kuwasaidia kupata misaada na kuwawezesha kuwa na maendeleo endelevu katika siku hii ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Vijana Duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 11 Agosti na kutimiza malengo aliyokuwa akiyatafakari baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere juu ya Vijana.
Umati wa wakazi wa Temeke katika tamasha la siku ya maadhimisho ya Kimataifa ya Vijana Duniani ambako zilifanyika shughuli mbambali ikiwemo Ujumbe kutoka Serikalini na Kupima virusi vya Ukimwi bure.

Baadhi ya Vijana wakitazama machapisho ya vijarida mbalimbali vinavyotoa taarifa kuhusiana na Afya zao na jinsi ya kupata huduma.

Mpiga picha Mkuu wa Mtandao wa habari wa MO BLOG Jofrey Mwakibete akipima Presha katika hatua za kuelekea kupima maambukizi ya VVU ikiwa ni kuhamasisha Vijana wenzake kujitambua kama wameathirika.

Mmoja wa wakazi wa jijini Dar es Salaam akicheki Afya yake.
Wakazi waliohamasika kupima VVU na magonjwa ya Zinaa wakiwa katika foleni ya kupata huduma hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya vijana Duniani katika viwanja vya Mwembeyanga Temeke jijini Dar.
Mpiga picha Mkuu wa Mtandao wa habari wa MO BLOG Jofrey Mwakibete akipima Virusi vya Ukimwi.
Mmoja wa wafanyakazi wa MO BLOG akipima VVU kujua kwamba poa au tayari.
Meza Kuu ikongozwa na Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel kwa niaba ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akikagua Timu ya soka ya Vijana ya Wanawake ya Evergreen kkutoka Temeke ambayo ilipambana na Timu ya Mburahati Queens kuonyesha ushirikiano wa Vijana akiwa ameambatana na Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Maria Khan na Mkurugenzi Mkazi wa AMREF Dkt. Festus Ilako.
Mheshimiwa mgeni rasmi hapa akikagua timu ya Mburahati Queens.
Pichani Juu na Chini Kipute kati ya Mburahati Queens na Evergreen Queens ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Evergreen kushinda 2-1.

Popular Posts