Pages

Tuesday, August 14, 2012

Rais Jakaya Kikwete Arejea Nchini Kutoka Ghana,Afuturu na Watoto Yatima na Walemavu

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakigawa zawadi kwa watoto yatima na walemavu waliohudhuria futari waliyowaandalia ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisoma barua aliyoandikiwa na mtoto Khaitham Jumbe(kulia) wakati wa futari aliyowaandalia watoto walemavu na yatima ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati anayeangalia ni mtoto Hamida Jacks mdogo wake Khaitham. Mtoto Khaitham Jumbe ni mlemavu wa ngozi na alikuja ikulu na wazazi wake.
Baadhi ya watoto yatima na walemavu wakishiriki katika futari ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik muda mfupi baada ya kuwasili akitokea nchini Ghana ambapo alishiriki mazishi ya aliyekuwa Rais wan chi hiyo Marehemu John Atta Mills. Kushoto ni Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali Davis Mwamnyange.Picha na Freddy Maro-IKULU

Popular Posts