Pages

Tuesday, August 14, 2012

TAARIFA YA SEKRETARIETI KUU TAWI LA CCM-AFRIKA YA KUSINI MWAKA 2012/2013

Ndugu wajumbe: Chama cha mapinduzi tangu kimeanzishwa hapa AFRIKA YA KUSINI kilikuwa na mikakati mbalimbali ya kichama ili kuweza kuhakikisha kuwa tawi linakuwa imara na hatimaye kuzidi kuimarisha chama kwa ujumla.vilevile napenda kusema kutokana na sera na itikadi za chama cha mapinduzi kwa kufuata katiba ya chama na taratibu tulizojiwekea katika chama ni msingi pekee tunajivunia kama chama cha mapinduzi katika kulinda na kutetea haki na maslahi ya chama kitaifa kwa pamoja.Mbali na jukumu hilo pia ni wajibu wa chama kusaidia wananchi kuelewa serikali yao kuwa inafanya kitu gani katika kuleta maendeleo ya taifa na hatimaye kuweza kupambana na adui mkubwa wa maendeleo katika nchi yetu ambae ni umaskini.

MAFANIKIO

Ndugu wajumbe wa kamati ya sias:, kiutendaji na katika kutekeleza majukumu ya chama cha mapinduzi katika tawi letu kumekuwa na mafanikio mbalimbali na makubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa tawi la chama cha mapinduzi AFRIKA YA KUSINI.Haya yote ni katika kutekeleza majukumu ya chama cha mapinduzi tangu kilipoanzishwa.

A.KUPATIKANA KWA WANACHAMA WAPYA.

Chama cha mapinduzi tawi la Afrika ya Kusini limeweza kupata idadi ya wanachama wapya kwa idadi ya kuridhisha sana kutokana na matokeo mazuri ya wanachama imepelekea tawi kuwa na idadi ya wanachama 130 kwa kipindi cha mwaka 2011/12.Vile vile jumuiya mbalimbali za ccm tawi AFRIKA YA KUSINI zimeweza kuhamasisha na kuwa na idadi kubwa ya wanachama katika jumuiya hizo.Hivyo basi napenda kutoa pongezi kwa jumuiya zote mbili kwa kazi nzuri waliofanya na wanayoifanya mpaka sasa kuhakikisha chama kinakuwa na wanachama wengi kuanzia ngazi ya tawi mpaka kwenye jumuiya zake.Napenda kusema kuwa mafanikio haya hayakupatikana hivi hivi bali kutokana na shughuli mbalimbali tulizoweza kuzifanya kupitia tawi na jumuiya zake kwa ujumla.Kwa mfano sherehe mbalimbali zilizofanyika kwa kipindi tofauti tofauti za kichama na jumuiya zimeweza kuhamasisha watu wengi kujiunga kutokana kazi nzuri tunayoifanya katika tawi.Hivyo basi napenda kutoa ombi kupitia tawi zoezi hili tunalolitumia mara



Popular Posts