Pages

Thursday, September 6, 2012

KARIBU SIKU YA MTANZANIA NCHINI MAREKANI

Mahali: Tanzania House,
1232 22Nd Street, N.W.
Washington D.C.; 20037
Tarehe: SEPTEMBA 15, 2012
Kiingilio: BURE
Muda: (Saa 4:00 asubuhi – Saa 12 Jioni)

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Washington D.C. unawakaribisha Watanzania wote waishio maeneo ya DMV (District of Columbia, Maryland na Virginia) na vitongoji vyake, kuhudhuria siku ya Mtanzania, ambapo Watanzania watashirikikwenye kuonyesha bidhaa, tamaduni, mila na desturi za Kitanzania kwa wageni (Wamarekani na wa Mataifa mengine) watakaotembelea ubalozini.

Madhumuni makuu ya Ubalozi kuandaa Siku ya Mtanzania kwanza ni kuwaelimisha wenyeji wa Marekani kuhusu Tanzania. Pili kuitangaza zaidi Tanzania kwa kuvutia watalii wengi kutembelea Tanzania. Tatu ni kutambulisha na kutangaza biashara mbalimbali na hudumazitolewazo na Watanzania waishio hapa Marekani.

Ubalozi unaomba Watanzania wenye bidhaa mbambali za Kitanzania, mapishi (wenye leseni),vikundi vya ngoma, muziki, mitindo, na Watanzania wenye kampuni za utalii, kujiandikisha ubalozini kuanzia tarehe 1 hadi 15 Agosti, 2012 kwa maandalizi ya siku hiyo.

Kwa Watanzania watakaopenda kujitolea kushiriki siku hiyo au kuonyesha bidhaa mbalimbali wajiandikishe kwa wafuatao:

Dkt. Suitbert Mkama
202 884 1087
Barua pepe smkama@tanzaniaembassy-us.org
Asia Dachi
202 884 1096
Rosemary Mziray
202 884 1081

Ubalozi unapenda kuwahamasisha Watanzania kuvaa vazi la Kitanzania

Karibuni Sanaa

Popular Posts