Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akikabidhi sehemu ya vifaa hivyo vya michezo kwa Makamu Mwenyekiti wa timu ya Simba,Geofrey Nyange Kaburu.Katikati ni Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba
Picha ya Pamoja:Toka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa timu ya Simba,Geofrey Nyange Kaburu,Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba,Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe na Afisa habari wa Timu ya Yanga,Luis Sendeu.
  Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akizungumza   na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya   kukabidhi vifaa vya micheko kwa timu za Yanga na Simba za jijini Dar es   Salaam iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka   nchini (TFF) Ilala.Kushoto ni Afisa habari wa timu ya Yanga,Luis  Sendeu  na kulia ni Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba.
  Meneja   wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akikabidhi sehemu   ya vifaa hivyo vya michezo kwa Afisa habari wa Timu ya Yanga,Luis   Sendeu.
Zikiwa zimebaki siku tisa kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi kuu Tanzania Bara 2012/2013, Kilimanjaro Premium Lager imezikabidhi timu za Yanga na Simba vifaa kwa ajili ya michuano hiyo.
Vifaa hivyo vimetolewa ikiwa ni sehemu ya udhamini wa jumla wa dola za Kimarekani milioni 3 (takribani TSh4bilioni) za kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager kwa timu hizo kongwe na zenye ushindani mkubwa na historia yakipee hapa nchini.Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na jezi, kaptula, soksi, vyatu vya mpira, bibs, mipira na mifuko.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, yaliyofanyika   katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Meneja wa   Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema:
“Ni dhahiri kuwa Simba na Yanga ni klabu kubwa zaidi nchini Tanzania na zote kwa pamoja zimetwaa ubingwa wa soka Tanzania Bara mara 40 (Yanga   mara 22 na Simba mara 18), jambo ambalo ni mafanikio makubwa sana kwa   timu hizi. Ni wazi kuwa hakuna timu nyingine iliyoweza kufikia historia   hii ya pekee hapa nchini na kama mdhamini mkuu wa timu hizi,  Kilimanjaro  Premium Lager imeona umuhimu wa kuziunga mkono klabu hizi  katika  jitihada zake za kutuletea tena ushindani wenye burudani.” Alisema.
Pazia la michuano ya kuwania ubingwa wa mpira wa miguu Tanzania bara kwa msimu wa 2012/2013 litafunguliwa rasmi Septemba 15 mwaka huu kwa jumla ya timu 14 kujitupa kwenye viwanja tofauti.
Kavishe   aliahidi kuwa kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager kitaendelea   kudhamini timu za Yanga na Simba kutokana na ukweli kwamba timu hizo   ndio zenye wapenzi wengi zaidi hapa nchini na zinazotoa wachezaji wengi zaidi katika kikosi cha timu ya taifa (Taifa Stars).
“Ushirikiano   kati ya Kilimanjaro Premium Lager na klabu hizi umejikita katika mambo   yanayotuunganisha kama vile ushirikiano, umoja na kujituma kufanya   kilicho bora. Tunaendelea kutimiza wajibu wetu kwa klabu hizi na tuko   tayari kupeleka mpira wa Tanzania kwenye kilele cha mafanikio,” alisema.




