Warembo   wa Redd's Miss Temeke, wakiwa mazoezini jana katika Club ya   TCC Chang'ombe , tayari kwa shindano lao litakalofanyika Septemba 21   mwaka huu.
VIMWANA   15 wa Redd's Miss Temeke, juzi wameanza rasmi kambi yao katika Club ya   TCC Chang'ombe tayari wa kinyang'anyiro cha kanda hiyo, kumrithi   mrembo Husna Twalib anayeshikilia taji hilo.
Warembo   hao ambao wameanza programu ya shoo kwa wiki hii, chini ya ukufunzi wa   Dickson Daud kutoka kikundi cha THT, wanatoka katika vitongoji vya   Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambapo kila sehemu wametoka warembo   watano ambapo washindi watatu wa kwanza watapata fursa ya moja kwa moja   kushiriki Redds Miss Tanzania 2012.
Warembo   hao ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester,   Catherine asumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu,   Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa   Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.
Temeke   imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia   warembo Happiness Sosthenes Magesse aka Millen mwaka 2001, Sylvia Remmy   Baham mwaka 2003 na Genevieve Mpangala.
 Lakini   pia imetoa warembo waliowahi kushika nafasi ya pili na tano bora  katika  Miss Tanzania ama Jokate Mwegelo, Irene Uwoya, Irene Kiwia,  Queen  David, Cecylia Assey, Sabrina Slim, Miriam Odemba, Ediltruda  Kalikawe  na Asela Magaka.
Mbali   ya Redd's, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na Dodoma Wine, gazeti   la Jambo Leo, Push Mobile, City Sports Lounge, 100.5 Times FM, Kitwe   General Traders na 88.4 Times FM. 
Warembo   wanaendelea na mazoezi na leo, Agosti 5 wanatarajia kutembelewa na  Miss  Tanzania 2010, Genevieve Mpangala ambaye pia ni Miss Temeke wa  mwaka  huo.