Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiifunga rasmi  Kambi ya Timu ya Soka ya Mkoa wa Kaskazini Unguja hapo katika Jengo la  Kituo cha Huduma Rafiki Mahonda. Kulia Ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na Ameir Katibu wa CCM Wilaya na  Kaskazini B. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa ZFA Wilaya ya Kaskazini “A”  Khamis Kombo. 
    Makamu wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi  Seif Ali Iddi akikabidhi mchango wa Shilingi 700,000/- kwa Mkuu wa  Msafara wa Timu ya Mkoa Kaskazini Unguja ambae pia ni Makamu Mwenyekiti  wa ZFA Wilaya ya Kaskazini B Omar Ali Khamis. Mchango huo ni kwa ajili ya ununuzi wa Viatu kwa Timu ya Soka ya Vijana  wa Mkoa huo watakaoshiriki Mashindano ya Copa Coca Cola Jijini Dar es  salaam yanayptarajiwa kuanza Mwishoni mwa Wiki hii.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na  Wana soka wa Mkoa wa Kaskazini Unguja  chini ya umri wa miaka 17 katika  hafla ya kuifunga rasmi kambi yao hapo katika Jengo la kituo cha Huduma  rafiki Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja. Timu hiyo inatarajia kuwa miongoni mwa wana michezo watakaoshiriki  kwenye mashindano ya Copa Coca Cola yatakayoanza Jijini Dara es salaa  Mwishoni mwa Wiki hii.