Pages

Tuesday, June 19, 2012

NAPE AMPASHA MBUNGE MSIGWA AMTAKA KUJIANDAA KUACHIA JIMBO 2015

katibu wa ikitadi na uenzi wa CCM Taifa Nape Nauye akiwahutubia wakazi wa jimbo la Iringa mji leo
Wananchi wakishangilia hotuba ya Nape
Nape akiwa na mwenyekiti wa CCm mkoa wa Iringa Deo Sanga (kushoto) na viongozi wengine wa wilaya ya Iringa na Kilolo
Nape akimsikiliza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ledian Mng'ong'o akielezea mazuri ya CCM
Mbunge Ritta kabati (kulia) akiwa na mbunge Lediana Mng'ong'o wakifuatilia hotuba ya Nape
Umati wa wananchi wakifuatilia hotuba ya Nape




katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha mapinduzi ( CCM) Taifa Bw. Nape Nauye amekiri kuwa CCM ilipoteza jimbo la Iringa mjini kwa makosa yake na kuwa kosa hilo kamwe halitarudiwa tena na kumfananisha mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa kuwa ni msindikizaji wa CCM katika jimbo hilo.

Kwani alisema kuwa kosa lililofanyika katika uchaguzi mkuu mwaka 2010 kwa kushindwa kuongoza kura za ubunge ni kutokana na makosa yaliyojitokeza hivyo kupelekea madiwani kushinda na Rais Jakaya Kikwete kupata ushindi mkubwa ila ubunge baada ya yule waliomchagua wana CCM Frederick Mwakalebela jimbo hilo lilichukuliwa na upinzani kosa ambalo kamwe halitarudiwa tena.

Asema vyama vya upinzani ni vyama vya wanaharakati kwa ajili ya kuikumbusha serikali ya CCM kwa pale inapokosea na sio kuja kuongoza nchi.

Pia Nauye aliuagiza uongozi wa serikali ya mkoa wa Iringa kuhakikisha unafungua mara moja barabara ya Magereza inayoelekea Hospitali ya mkoa ambayo imekuwa ikichangia usumbufu wa wagonjwa Kwenda kutibiwa.

Akiwahutubia wakazi wa jimbo la Iringa mjini katika viwanja vya Soko kuu Leo ,Nauye alisema kuwa moja Kati ya kilio kikubwa kwa wakazi wa mji wa Iringa ni hatua ya uongozi wa Magereza Iringa kuifunga barabara hiyo kwa ajili ya matumizi ya Magereza mkoa wa Iringa jambo ambalo linasababisha usumbufu kwa wananchi wanaofika Hospitali hiyo ya mkoa.

Hivyo alisema tayari amemwagiza mkuu wa mkoa wa Iringa DKT Christina Ishengoma kuhakikisha anasimamia zoezi hilo ili barabara hiyo ifunguliwe na kupunguza kero za wananchi na wagonjwa wanaofika kutibiwa katika Hospitali hiyo ya mkoa.

Aidha Nauye amewacharukia madaktari wa Hospitali za umma ambao wameendelea kuichafua serikali iliyopo madarakani kwa kushindwa kutoa dawa kwa wagonjwa na kuwaelekeza maduka yao kwa ajili ya kununua dawa hizo.

Alisema kuwa kumekuwepo na utaratibu mbaya kutoka kwa baadhi ya madaktari na wauguzi kushindwa kuwapa dawa wagonjwa wanaofika kutibiwa na badala yake kuwaandikia dawa hizo na kuwaelekeza maduka ya Kwenda kununua dawa hizo maduka ambayo yanamilikiwa na madaktari hao.

Hivyo alitaka madaktari wanaofanya hivyo kuacha Mara moja Kwani kuendelea kufanya hivyo ni kuwanyanyasa wananchi hao ambao wanafika kutibiwa.

Akielezea kuhusu bajeti ya mwaka 2012/ 2013 Nauye alisema kuwa bajeti ya serikali ya sasa imepunguza utegemezi kutoka asilimia 42 hadi asilimia 26 pekee hivyo aliwataka wapinzani kuacha kufuru kwa kuponda bajeti hiyo.

Alisema kuwa katika bejeti ya miaka ya nyuma ilikuwa haiweke bajeti ya ndani ila kwa sasa serikali imetenga bajeti ya maendeleo zaidi ya trioni 2 ambayo pia wapinzani walipaswa kuizungumza badala ya kuendelea kukosoa hata pale serikali inavyofanya vema.

Pia alisema kuwa vyama vya upinzani vinapaswa kuendelea kusema unwell zaidi badala ya kuendelea kufanya siasa ya kudanganya umma wa watanzania kwa mambo ambayo yanaukweli .

Katika hatua nyingine Nauye alivitaka vyama vya upinzani kuendelea kuifanya kazi ya katakana CCM huku CCM ikiendelea kuchapa kazi na kudai kuwa vyama vya Upinzani ni sawa na kuku wako kumshikia manati na kudai kuwa wapinzani wote walitoka CCM hivyo iwapo CCM wachafu hata wao wamegoma huku.

Kwa upande wake mstahiki meta wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi alisema kuwa uongozi wa Manispaa ya Iringa umeendelea kujenga barabara za mji huo katika kata zote 14 ikiwa ni pamoja na kuendelea na kuboresha huduma za afya.

Alisema kuwa kutokana na msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa uongozi wa Manispaa ya Iringa ulimwomba Rais Jakaya Kikwete kusaidia kiasi cha shilingi milioni 600 ambazo zimefanikisha ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Iringa eneo la Frelimo ,Hospitali ambayo imeanza kazi.

Popular Posts