Pages

Tuesday, June 19, 2012

Maelezo ya Bajeti Kivuli

Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.

MAPATO

SHILINGI MILIONI

A Mapato ya ndani

11,889,078

i)mapato ya kodi (TRA)

10,232,539

ii)Mapato yasiyo ya kodi

1,163,533

B Mapato ya Halmashauri

493,006

Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani.

Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.

Kabwe Zuberi Zitto,Mb

Waziri wa Fedha na Uchumi Kivuli

19.06.2012

Popular Posts