Kaka mkubwa wa marehemu aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward 
Ogunde,  George Ongiri Ogunde (wa kwanza kulia) akishirikiana na ndugu, jamaa na  waandishi wa habari, kubeba mwili wa mhariri huyo, aliyefariki dunia  ghafla jana usiku eneo la Forest Hill, mjini Morogoro. Mwili huo ulikuwa  unatolewa chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa  Morogoro kwa ajili ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa  maandalizi ya mazishi katika Kijiji cha Mugumu kilichopo wilaya ya  Serengeti, mkoani, Mara.. 

Mbunge  wa Jimbo la Morogoro, Azizi Abood, akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Kampuni ya New Habari (2006), Husein Bashe wakisubiri kuuona mwili wa  Willy Edward

Baadhi  ya waandishi wa habari akiwemo Mbunge wa Morogoro mjini, Azizi Abood,  wakiwa na huzuni walipokuwa wakisubiri kutoa heshima za mwisho katika  Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, muda mfiupi kabla ya mwili kusafishwa  Dar es Salaam.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa kaka mkubwa wa
Ogunde muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kwenda jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mazishi katika kijiji cha cha Mgumo kilichopo wilaya ya Serengeti mkoani Musoma. Wa pili kutoka kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Morogoro, Alfred Shao na kaka mkubwa upande wa baba, Isack Ugunde
marehemu aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Ogunde, George Ongiri 