Pages

Tuesday, June 19, 2012

Mkurugenzi Mkuu wa Zamani wa Bodi ya Utalii Tanzania Peter J Mwenguo Afariki Dunia

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania Bwana Peter J Mwenguo
--
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania Bwana Peter J Mwenguo amefariki dunia tarehe 18 Juni 2012 saa nne asubuhi katika Hospitali ya Muhimbili .
Bwana Peter Mwenguo aliajiriwa na Bodi ya Utalii tarehe 22 0ktoba 1993 kama Mkurugenzi wa Masoko na kupandishwa cheo kuwa Mkurugenzi Mwedeshaji kuanzia tarehe 6 Februari, 1999 mpaka tarehe 22 Oktoba, 2008 alipostaafu kwa mujibu wa sheria na baadaye kufanya kazi kwa mkataba hadi tarehe 20 Desemba 2009. Bwana Peter. Mweguo amefanya kazi Bodi ya Utalii zaidi ya miaka 15.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake katika Magorofa ya TRA, Mwenge, Dar-es-Salaam. Taarifa kuhusu siku na mahali pa Mazishi zitatolewa baadaye.

Mungu ailaze roho ya marehemu Bwana Peter Mweguo mahali pema peponi ! Amen

Popular Posts