Pages

Sunday, June 17, 2012

Uzinduzi wa Madrasat Nurullah Kitope Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya ufunguzi wa madrasat Nurullah Kitope Zanzibar,iliyopo Wilaya ya Kaskazini B Unguja,Mkoa wa Kaskazini,(kulia) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar,pia Mwakilishi wa jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi,jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa Abdallwa Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi wa mwakilishi wa Jimbo la Uzini CCM Mohamed Raza
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza,akitoa shukurani zake na kwa niaba ya wafadhili waliojenga Madrasat Nurullah,baada ya kufunguliwa rasmi jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein, huko Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akifuatana Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar,pia Mwakilishi wa jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi,pamoja na viongozi wengine alipowasili katika Jengo la Madrasat Nurullah Kitope,kwa ajili ya kulifungua rasmi,lililojengwa kwa ufadhili wa Abdallwa Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi wa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza.
Baadhi ya wanafunzi wa Kike wa Madrasat Nurullah ya Kitope wakiwa katika sherehe ya ufunguzi wa madrasa yao iliyojengwa kwa kiwangi kizuri ambacho kitwafanya kuwa na arizaidi ya kusoma kwa bidii,iliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,iliyojengwa kwa ufadhili wa Abdalla Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi wa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza.Picha na Ramadhani Othman,IKulu-Zanzibar

Popular Posts