Pages

Monday, June 18, 2012

JAJI WARIOBA KUKUTANA NA WAHARIRI

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba kesho, Jumanne, Juni 19, 2012 atakutana na
Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam kuanzia saa
3:00 asubuhi - 7:00 mchana kwa lengo la kuzungumza nao kuhusu kazi ya
ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya.


Mkutano wa aina hiyo pia utafanyika mjini Zanzibar
katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani keshokutwa Jumatano, Juni 20, 2012, kuanzia saa
3:00 asubuhi kwa Wahariri waliopo Zanzibar. Pamoja na Mwenyekiti wa Tume, katika mikutano hiyo
ya wazi kwa Waandishi wa Habari pia watakuwepo Wajumbe wengine wa Tume.

Katika mikutano hiyo, Mwenyekiti wa Tume atafafanua
kazi za Tume, kama zilivyoainishwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura
ya 83 na namna Tume inavyozitekeleza.

Tume ya Mabadiliko ya
Katiba imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, na
Wajumbe wake waliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe
6 Aprili na aliwaapisha tarehe 13 Aprili mwaka huu. Tume ilianza kazi rasmi
tarehe 1 Mei, 2012.

Popular Posts