Waziri  wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Mhe, Fatma Abdulhabib Fereji 
  --- 
   Waziri  wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Mhe, Fatma Abdulhabib Fereji  amesema kuwa ukataji wa miti ovyo husababisha uharibifu mkubwa wa  mazingira  jambo ambalo hufanywa na wananchi wa Zanzibar  hususan akinamama ndio wachangiaji wakubwa kutokana na kuwekeza maisha  yao katika kilimo cha mwani.
  Aliyasema  hayo huko katika ukumbi wa baraza la Wawakilishi nje kidogo na mji wa  Zanzibar alipokuwa akijibu suala la Mhe. Salehe Nassor Juma aliyetaka  kujua wizara  inampango gani wa kutoa utaratibu mbadala  kwa kinamama  kuweza kuwapatia njia bora ya  kufungia kamba zao za mwani badala ya  kutumia miti .
   Alisema  kwamba anakiri kuwa akinamama wengi wameweza kujiajiri wenyewe katika  kilimo cha mwani kazi hiyo ndio inayowawezesha kujikimu kimaisha hivyo  suala la kuwakataza akinamama hao kwa ghafla bila ya kuwapatia njia  nyengine ya kutumia itakuwa ni gumu kwa wizara hiyo ikizingatia ni  sehemu moja ya maisha yao .
   Aidha  alisema kuwa serikali kupitia taasisi zake zikiwemo wizara ya Mifugo na  Uvuvi ,Kilimo na Mali asili pamoja na Ofisi ya Makamo ya Kwanza wa Rais  ziliweza kupanga mipango maalum  ambayo itaweza  kuwapatia mbinu   endelevu ambayo haitoweza kuathiri miti ambayo wakulima wa mwani kuacha  kutumia miti 
    ya asili.
  Na 
   Khadija Khamis –Maelezo-Zanzibar