Pages

Saturday, July 14, 2012

KUHUSU MAFAO YA PENSHENI KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO

Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu ombi lililotolewa na Katibu wa Tamico
(Geita) kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu mafao

· Ni kweli kuwa Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na
Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13
Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na
imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini
mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.

· Kwa mujibu wa marekebisho hayo mafao ya kujitoa (withdrawal
benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa
yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko
atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka
55) au kwa lazima (miaka 60).

· Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili
kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa
mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya
uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya
kujitoa yanapunguza kama si kuondoa kabisa kinga hii ya mfanyakazi
anapofika uzeeni.

· Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao
ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa
kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu
tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu
kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena
muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na
Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika

· Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi
kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi
watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa
hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria.
Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya
wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi
na waajiri ili kupata maoni yao.

· Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama
yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo.

Imetolewa na Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii.

KWA UFAFANUZI HUU TOKA MAMLAKA HUSIKA,

(i) Hakuna shaka kwamba sheria tayari imeaanza kutumika.

(ii) Hakuna shaka kwamba Bunge na Serikali wamekaa kimya kwa sababu wanajua
kwamba sheria waliyotunga na kupitisha ni pigo kwa wafanyakazi hawa wa
sekta binafsi hasa ukizingatia kwamba

- sekta binafsi ndo wachangiaji wakubwa wa mifuko hiyo.

- Usalama wa Ajira wa wafanyakazi wa sekta binafsi ni asilimia zero maana
waajiri wamekuwa wakiwafukuza kama Popo au senene.serikali hajaiweka kinga
madhubuti kwa wafanyakazi hawa.sheria ya kazi iliopo inawasaidia zaidi
waajiri.

- Mazingira ya kazi kwa sekta binafsi sio rafiki kwa afya na usalama wa
wafanyakazi.Hivi unategemea kijana aliye na miaka 25 kwa sasa na anafanya
kazi migodini,viwanda vya chuma,Ujenzi NK afanye kazi hadi astaafu kwa
mazingira haya? NADHANI HUU NI UVIVU WA KUFIKIRI KWA WATU TULIOWAPA DHAMANA
KUBWA NA HILI NASEMA HALIKUBALIKI HATA KIDOGO!!!!!!!!!!!!!!!!!

NINI KIFANYIKE?

TUNASUBIRI MAJIBU TOKA SERIKALINI NA BUNGENI

Kama kweli wametunga na kupitisha sheria hii kandamizi,nasema kitu hiki
hakikubaliki hata kidogo.Nguzo ya wafanyakazi ni UMOJA NA
MSHIKAMANO.Wafanyakazi wote sekta binafsi tutapiga kura ya maoni kukataa
sheria hii kisha tutapeleka suala hili mahakamani na iwapo mahakama itaamua
ndivyo sivyo nadhani hatua itakayofuata ni kuprotest against this ACT.

Nimeguswa sana na Jambo hili kwa sababu Sheria hii imetungwa kukandamiza
masilahi ya wafanyakazi wanyonge wa nchi hii na kwa pamoja tutahakikisha
sheria hii inafutwa hata kama watatu Kolimba,mwakyembe,ulimboka NK.

MSHIKAMANO DAIMA - SOLIDARITY FOREVER

Benjamin Daudi Dotto

Katibu wa Tamico wilaya ya Geita,

SLP 335,

Geita – Tanzania.

Simu: ofisi +255 774 866635

Simu:mkononi + 255 767 715116 alt.+255 784 715116

Popular Posts