
  Mbunge wa  Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji  akimpongeza Dr. Asha Rose Migiro kwa  kazi nzuri alipokuwa akitumikia kama Naibu  Katibu Mkuu wa Umoja wa  Mataifa  walipokutana leo katika Uwanja wa ndege.
 
 Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini  Dr. Alberic Kacou (katikati) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere kumpokea Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa  Mataifa Dr. Asha Rose Migiro aliyemaliza muda wake leo wakati akirejea  nchini Tanzania. Kushoto ni Afisa wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa  nchini Hoyce Temu.
 
  Baadhi ya Mabalozi, Wahadhiri na  Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na wafanyakazi wa  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa wamejipanga  kumpokea Dr. Asha Rose Migiro.
 
  Msafara wa Dr. Asha Rose Migiro  ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Mh. Benard Membe (gari la  pili) kuelekea sehemu maalum ya mapokezi.
 
 Dr. Asha Rose Migiro akishuka kwenye gari yake baada ya kukanyaga Ardhi ya Tanzania.
 
 Dr. Asha Rose Migiro akipokelewa kwa  shangwe na zawadi za  maua kutoka kwa ndugu, jamaa, marafiki na  wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje waliofika kumlaki.
 
 Dr. Asha Rose Migiro akisalimiana na  baadhi ya mabalozi wapya walioteuliwa na Mh. Rais hivi karibuni. Kushoto  ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.
 
 Dr. Asha Rose Migiro akiendelea  kusalimiana na  Baadhi ya Mabalozi. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe sambamba na Mratibu Mkazi wa  Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.
 
 Waziri Membe na Dr. Migiro wakielekea kwenye chumba maalum cha mapumziko kabla ya mkutano na waandishi wa habari.
 
 Dr. Asha Rose Migiro (katikati),  akizungumza na waandishi wa habari nchini Tanzania baada ya kumaliza  muda wake kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambapo pamoja na  mambo Mengi amesisitiza kwamba hatojihusisha na siasa kwa sasa. Kushoto  ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe  na Kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.
 
 Dr. Asha Rose Migiro akisisitiza jambo  wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya kutua katika uwanja wa  ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere. Kushoto ni Waziri wa Mambo  ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe.
 
 Dr. Asha Rose Migiro (katikati) akiteta  jambo Waziri Membe sambamba na Viongozi mbalimbali wa Mashirika ya Umoja  wa Mataifa nchini wakiongozwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa  nchini Dr. Alberi Kacou (kushoto) waliofika kumlaki katika Uwanja wa  Ndege wa Mwl. J.K Nyerere.
 
 Pichani Juu na Chini ni wakinamama  wakimwimbia Happy Birthday Dr. Asha Rose Migiro ikiwa ni maadhimisho ya  siku yake ya kuzaliwa aliporejea nyumbani leo.
 

 Kikundi cha Ngoma kikitoa burudani kwa Dr. Migiro (hayupo pichani)
 
 Dr. Asha Rose Migiro akizungumza Jambo  na Dr. Alberic Kacou wakati wakitizama burudani ya ngoma iliyoandaliwa  maalum kwa ajili yake. Kushoto ni Waziri Membe.
 
 Dr. Migiro akiwasalimia  wasanii wa kikundi cha ngoma.
 
 "Karibu tena Nyumba Mama"... Waziri Membe akiagana na Dr. Asha Rose Migiro baada ya mapokezi.
 
 Dr. Asha Rose Migiro akiagana na  Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou.
 
 Dr. Asha Rose Migiro akiondoka katika  uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere sambamba na ulinzi  mkali wakiwemo maafisa wa kimataifa kutoka Ufilipino waliohakikisha  ametua nchini Salama.
  -- 
  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  (UN) ambaye amemaliza muda wake, Dk. Asha Rose Migiro, amerejea nyumbani  leo na kusema kwamba anatarajia kurudi kufundisha katika Chuo Kikuu cha  Dar es Salaam ambako alikuwa akifundisha kabla ya kuingia kwenye ulingo  wa siasa.
  Kinyume na matarijio ya watu wengi, Dk.  Migiro amesema kuwa kwa sasa hatarajii kujishughulisha katika mambo ya  siasa na wala hana mipango ya kugombea urais siku za mbele.
  Amesema kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa  Mataifa, Ban Ki-Moon, amamteua kuwa Balozi Maalum wa Malaria katika Bara  la Afrika na kuongeza kuwa pamoja na kwamba shughuli hizo atakuwa  anazifanya kwa muda wake mchache, bado kuna uwezekano mkubwa zikambana  na kushindwa kujishughilisha na mambo ya kisiasa.