Pages

Tuesday, July 31, 2012

Bondia Mtanzania Selamani Kidunda Akiwa na Wadau Mbalimbali Muda Mfupi Baada Ya Kudundwa na Bondia BELOUS Vasilii toka Moldova kwa point 7-20.

Bondia Kidunda, mdau wa michezo Magesa na kiongozi wa msafara wa Tanzania Jarufu wakiwa kwenye basi la wanamichezo kurudi kambini.
Baadhi ya viongozi wa michezo walioko London, kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa michezo nchini Ndg.Thadeo, Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Ndg.Gullam, Makamu wa Rais wa Kikapu Tanzania Ndg.Magesa na Kiongozi wa msafara wa timu ya Tanzania Ndg. Jarufu.
Bondia wa Tanzania Selamani Kidunda mwenye fulana nyekundu akiwa na viongozi na baadhi ya wadau wa michezo wakati akienda kupigana na Bondia toka Moldova BELOUS Vasilii, Kidunda alipoteza mchezo huo kwa point 7-20.
Wadau wa michezo walioko London, kutoka kushoto Ndg. Amosi Msanjila afisa wa ubalozi London, Mtangazaji maarufu wa BBC Ndg. Charles Hilary, Makamu wa Rais wa TBF Ndg. Phares Magesa, na Mchambuzi mahiri wa Michezo wa BBC na mmliki wa tanzaniasports.com Ndg. Israel Saria.
--
Bondia pekee anayeiwakilisha Tanzania kwenye michezo ya Olimpiki Selemani Kidunda amepoteza mchezo wake Jana dhidi ya Bondia BELOUS Vasilii toka Moldova kwa point 7-20.

Tanzania itajaribu tena bahati yake tarehe 31/07/2012 wakati muogeleaji wetu wa kiume Ammaar Ghadiyali atakapocheza mchezo wake, tumuombee kila la heri kijana huyo atuwakilishe vyema.

Popular Posts