Pages

Wednesday, August 1, 2012

WAZIRI MKUU KUZINDUA KITABU CHA WANASAYANSI WA TANZANIA KIITWACHO “LIGHTING A FIRE”

Siku ya Alhamisi 2 Agosti 2012, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb.), atazindua kitabu kiitwacho “Lighting a Fire”ikimaanisha “Kuwasha Moto”. Ndani ya kitabu hicho kuna maelezo ya kusisimua kuhusu wanasayansi 31 mabingwa wa Kitanzania. Kitabu hiki ni cha kwanza katika mfululizo wa taarifa zenye kuelimisha na kinaelezea safari ndefu za wanasayansi hao na mchango wao kitaaluma katika maendeleo ya nchi yetu. Madhumuni ya kitabu hiki ni kuondoa kasumba iliyojengeka juu ya ugumu wa kusomea sayansi, na kinahamasisha vijana wetu wa kiume na kike, wachukue masomo ya sayansi, wayapende na wayachangamkie katika kulitumikia taifa katika fani ya sayansi, hasa katika karne hii ya 21 ya sayansi na teknolojia.

Uzinduzi huo utafanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) uliopo Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Kijitonyama, kuanzia Saa 4:00 asubuhi. TAAS ni mkusanyiko au jumuiya ya wasomi wa sayansi na haina nia ya kutafuta faida/fedha. TAAS iliundwa tarehe 24 Februari 2004. Madhumuni yake ni kuendeleza na kukuza matumizi ya sayansi na technologia kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania kwa ujumla.

Kazi za TAAS ni pamoja na:kuendeleza, kukuza na kubuni mikakati ya elimu ya sayansi na sosiologia kiuchumi, kushauri na kutoa mikakati ya kuboresha sera katika sayansi, technologia na ubunifu kwenye jamii, kufadhili na kuwezesha elimu ya sayansi na teknologia kwa utafiti wa hali ya juu na matumizi yake kwa kulipia gharama za utafiti kiushindani na kukuza miradi ya utafiti, kuwezesha ubadishanaji wa mawazo na mijadala kwa kutumia majarida ya kisayansi, mikutano, warsha na mihadhara, kuboresha mfumo wa sayansi kwa kuboresha “sera” viwango ya kisayansi kitaifa, kwa kuboresha sera ya elimu ya sayansi nchini pamoja na walimu wa sayansi, kuwezesha uongezekaji wa mahusiano (linkages) na washiriki wa jumuia ya kisayansi nje ya nchi kwa kubadilishana mitaala, na kufadhili elimu ya ufundishaji na utafiti.

Hafla hiyo itakamilishwa kwa kutambulishwa rasmi kwa wajumbe wapya wa Kamati Kuu ya Utendaji ya TAAS waliochaguliwa hivi karibuni kama ifuatavyo:

1. Prof. Esther Mwaikambo - Rais wa TAAS
2. Prof. Joseph Kuzilwa - Makamu wa Rais
3. Dr. Gratian R. Bamwenda - Katibu Mkuu
4. Dr. Roshan Abdallah - Naibu Katibu Mkuu
5. Prof. Bruno Ndunguru - Mweka Hazina
6. Prof. Ludovick Kinabo - Mhariri Mkuu
7. Prof. Matthew Luhanga - Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
8. Prof. Keto Mshigeni - Mjumbe wa Kamati ya Utendaji

Waandishi na vyombo vyote vya habari, wananchi na taasisi mbalimbali mnakaribishwa kuhudhuria hafla hiyo.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Bibi Isabela Seme Ndatu, Afisa Tawala, TAAS
Jengo la COSTECH, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi
S L P 33654, Dar es Salaam, Tanzania.
Simu: 255 22 2700747; Fax/simu: 255 22 2772974 Mob.: +255 767 619 991
e-mail: info@taas.or.tz; isabela_seme@yahoo.com

Popular Posts