Mama Maria akimkabidhia funguo za trekta moja kati ya kumi  aliyokabidhi, mmoja wa wakulima hao Sheikh Hamis Haji ambaye pia ni  Sheikh wa Kata ya Kwadelo.
  Mkazi  wa kijiji cha Kwadelo, Maulid Msema akipokea funguo moja kati ya 10 za  Matrekta yaliyokabidhiwa na Mama Maria Nyerere kwa ajili ya wakulima wa  kijiji hicho  kilichopo wilayani  Kondoa, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo kijijini hapo,  katika hafla iliyofanyika Msasani jijini Dar es Salaam jana. Kushoto  anayeshuhudia ni Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omari Kariati.  Kisha Kariati akamkabidhi zawadi ya Kitenge Mama Nyerere kama shukurani  ya wananchi wa Kwadelo kujengewa kisima cha maji na baba wa Taifa  Mwalimu mwaka 1961 ambacho hadi sasa kipo.
   Halafu akamkabidhi mkoba wa safari kama akitaka kwenda Butiama
   Kariati akizungumza neno la kufungua shughuli. Kulia ni Mama Nyerere
  Mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Maria Nyerere, akimkaribisha,  diwani wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya KLondoa mkoa wa Dodoma, Alhaj Omar  Kariati, wakati diwani huyo na ujumbe wake wa wakulima kumi, walipofika  nyumbani kwa Mama Nyerere kwa ajili ya kukabidhiwa trekta kumi kwa  wakulima hao, katika sherehe iliyofanyika nyumbani kwa Mama Maria  Nyerere, Msasani jijini Dar es Salaam, jana.